MANISPAA YA ILALA YAFANYA MABORESHO MAKUBWA KITUOCHA AFYA BUGURUNI.
Na.John Luhende
Mwambawahabari
Katika kuboresha huduma za Afya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mwaka huu wa Fedha 2018/2019 imejipanga kukarabati kituo cha Afya buguruni ambapo imetenga jumla ya shilingi Milioni 79 kwajili ya ukarabati huo.
Akizungumzia ujenzi huo Mganga Mkuu wa Manispaa ya hiyo Emili Lihawa amesema , Pamoja na kiasihicho cha fedha pia Halmashauri imepokea jumla ya shilingi milioni 500 kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI kwaajili ya kuendeleza upanuzi wa kituo hicho ambapo watapanua jengo la X-RAY, UTRA-SOUND ,Upasuaji ,jengo la wazazi , na Jengo la Upasuaji dharua na Jengo la ufuaji wa nguo (Laundry).
Dkt Lihawa amesema ,ujenzi huo uko katika hatua mbalimbali za ujenzi ambapo Jengo la X-RAY pamoja na jengo la upasuaji yako katika hatua ya Linta ,Jengo la akimama liko katika hatua ya msingi na kupandisha kuta huku jengo la Ufuaji nguo (Laundry)likiwa katika maandalizi ujenzi.
Kutokana na ufinyu wa eneo hilo Dkt Lihawa amesema, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ,awali ilinunua baadhi ya maeneo ya wananchi wanao zunguka eneo hilo kwa kuwalipa fidia ambapo eneo hilo kwasasa ndiyo linalotumika kufanya upanuzi wa kituo hicho,na kuongeza kuwa kwasasa wanampango wa kuongeza eneo natayari nyuba saba zimeainishwa kulipwa fidia ambapo inakadiliwa jumla ya shilingi milion 500 zitatumika.
Pamoja na hayo Dkt Lihawa amewataka wananchi na wadau wa Afya kuunga mkono ujenzihuo kwa halinamali.
Post a Comment