KAMBI YA UPINZANI YAZIDI KUBOMOKA VINGUNGUTI , WENYEVITI WA SERKALI ZA MITAA ,MITAA SABA WAJIUNGA CCM.
Na.John Luhende
Mwamba wa habari
Kampeni za udiwani kata ya Vingunguti
zimechukua sura mpya baadaya wenyeviti wa Serikali za mitaa saba
kutoka CHADEMA na CUF kata ya vingunguti kujivua nyadhifa zao na kujiunga
na chama cha Mapinduzi CCM wakisema wanamuunga mkono Mgombea wakiti cha udiwa
kupitia CCM Omary Kumbila moto.
Wenyeviti hao wametangaza uamuzi
huo katika mkutano wakampeni uliofanyika vingunguti Relini , wakizunguza baada ya kukabidhi
kadi zao kwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Kate Kamba ,wamesema
wameamua kujiunga na CCM baadaya
kuchoshwa na migogoro isiyoisha katika vyama walivyotoka .
“Baba yangu Kumbilamoto uliniachia
mzigo takribani mwezi mzimmoja nilikuwa
nashinda ndani kuepuka lawama kwanini Omary Kumbilamoto kaondoka na sharifu
Mbulu ndiye mlinzi wake? naminimeamua
kuacha vyote katika chama cha wananchi CUF na nimeamua kujiunga rasmi na CCM’’ amesema
Aliye kuwa makamu katibu mkuu wa Chama
Cha wananchi CUF Julius Mtatiro amewataka wananchi wa vingunguti
kumchagua OMary kumbilamoto kwa kwakuwa
alifanya uamuzi sahihi kujiunga na ccm , amesema ,vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu uliopita vilikuwa vinadaii
serikali haitimizi wajibu wake kwa kuwa kulikuwa na ufisadi mkubwa
lakini sasa Serikali imefanyia kazi mambo yote chini yaMhe. Rais Dkt
John Pombe Magufuli
‘’vijana naomba tumuunge mkono kwa kumchagua omary Kumbilamoto kwa nafasi
hii ya udiwani nakukumbuka waka 2015 nilisima katika viwanja hivi kumuuombea
kura na shukuru mlimchagua nawaombeani
tena tumchague, amesema Mtatiro.
‘’Nataka niwaambie kitukimoja kuwa ,
Kumbila moto alikuwa hapa kama Diwani lakini nilikuwa siwezi kushirikiana
kwa sababu kunamambo mengine tukiyapanga kwenye chama chetu ya Ilani ya
chama yeye alikuwa na Ilani yake ya CUF,kwahiyo
nikiwa naye katika vikao vya maendeleo
tunakuwa tunapishana , na kwasababu kaona kunaspidi ya Rais ya kufanya kazi na maendeleo yanayo onekana
kwa macho na kuona nibora kujiunga na CCM ilikuhakikisha
wananchi wa Vingunguti , naomba tumchague, amesema Kalua.
Naye mgombea kiti cha udiwana kupitia CCM , Omary Kumbilamoto akiomba kura kwa
wananchi hao , ameahidi kuwasaidia walemavu kupata mikopo inayotolewa na
Halmashauri ili waweze kuanzisha biashara .
‘’Naomba niwahakikishie kuwa nikipita
walemavu wote tukutane katika ukumbi
wa Mashujaa ili niwatambue muweze kupata
asilimia 2 zenu za mkopo, amesema Mgombea.
Pamoja nahayo ameeleza kuwa ahadi ya kununua gari la waojwa katika zahanati ya Vingunguti
aliitimza na kwamba maneno yanayo enezwa na wapinzani wake kuwa Gari
alinnunuiwa na chama si za kwali na zianapaswa kupuuzwa .
‘’ Nawahakikishia kuwa gari hilo (AMBULANCE) nilinunua kwa pesa yangu na nakala za kadi hizi hapa zina jina langu wasiwadanganye‘’ alisema na kugawa nakala ya
kadihiyo ili wananchi wasome.
Post a Comment