GWAJIMA AMSHAURI LOWASA KUSTAAFU SIASA ILI KULINDA HESHIMA YAKE
Kada wa CCM Ndugu Methusela Gwajima, amemshauri Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Mheshimiwa Edward Lowasa Kustaafu rasmi harakati zake za
kisiasa na hasa siasa za majukwaa ili kulinda heshima yake.
Gwajima amesema ,Kipigo cha Monduli alichopata ni kibaya mno
na ni zaidi ya Kipigo Cha Mbwa Koko kiasi
kwamba, kisiasa sasa anatia aibu/Huruma/Simanzi,
hivyo anapaswa kusoma alama za
nyakati kwani kama ni kuisoma namba hakika hii ya Monduli ni ya kufunga mwaka !!
“Hivi kweli kama
umeweza kushindwa kulikomboa Jimbo moja tu
tena la Nyumbani kwako, Je utaweza tena kuhimili mchaka mchaka wa nchi nzima ? Kwa hakika busara ya kawaida
inakutaka upumzike na ikibidi uachane kabisa na harakati za kisiasa, baki
nyumbani walau hata uwe mshauri tu kwa watu watakaohitaji ushauri
wako” alisema Gwajima.
Gwajima ambaye ni Mwanasheria kitaaluma amemtaka Lowasa Kuepukana
na washauri wabaya waliomzunguka kwani
kwa mara nyingine tena wamefanikiwa kumuingiza chaka
bure mzee wa watu.
“Nadhani, Mhe. Lowasa amezungukwa na genge la wahuni na wapiga dili ndio maana wanashindwa
kumpatia ushauri mzuri unaoendana na umri na heshima yake.
Mhe. Gwajima amewapongeza
wagombea wote wa CCM waliofanikiwa kupata ushindi wa
kishindo
“Hongera sana wanaukonga, Hongera sana wana Monduli, Hakika
nyinyi hampangiwi cha kufanya ama kweli
wanaukonga na Monnduli sio wa
mchezo mchezo”
Mhe. Gwajima
amevipongeza vyombo vyote vya
dora kwa kusimamia amani na utulivu wakati wote wa kampeni na hatimaye katika
zoezi zima la uchaguzi.
Ushindi huu wa CCM katika chaguzi ndogo zilizofanyika jana ,ni
ishara kubwa ya imani walionayo wananchi kwa serikali yao chini ya Mhe. Raisi
wetu Mpendwa Dr. John Pombe Magufuli katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.
Mhe. Gwajima amepongeza
Mh. Raisi Magufuli kwa kufanya
mambo makubwa ya wakuwaletea wananchi maendeleo katika sekta zote na mda mfupi
sana tangu aingie madarakani.
Mhe. Gwajima Alimpongeza Rais Magufuli kwa ujasiri wake na usimamizi katika
kusimamia yafuatayo:
i.
Katika
Ujenzi wa Bomba la mafuta HOIMA –TANGA
ii.
Ongezeko
Katika makusanyo ya kodi –TRA
iii.
Mradi
wa STIEGLERS’S GORGE MEGAWATI - 2,100
iv.
Mahakama
wa rushwa na uhujumu uchumi
v.
Serikali
kuhamia makao makuu DODOMA
vi.
Elimu
bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne.
vii.
Ujenzi
wa Ukuta wa kulinda Madini MERERANI.
viii.
Kufufua
Shirika la ndege nchini.
ix.
Usajili
wa kuwatambua rasmi wamachinga 20,000
x.
Huduma bora za tiba kwa watanzania
xi.
Mafanikio
makubwa katika ujenzi wa miundombinu mfano mzuri ni Flying Over ya Tazara.
Mwisho Mh. GWAJIMA amewaomba watanzania kuendelea kumunga
mkono Mh. Raisin a serikali yake kwa ujumla KWANI YAJAYO YANAFURAISHA MNO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
GWAJIMA, MWANASHERIA NA KADA WA CCM
Post a Comment