ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA.
Mkurugenzi wa TIC Mwambe akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kampuni tano kutoka Korea Kusini na China wameonesha nia ya kuwekeza kwa kujenga viwanda vya kutengeneza madawa na vifaa tiba hapa nchini.
Makampuni hayo wameonyesha nia ya kuwekeza baada ya Mkurugenzi wa TIC kwenda nchini Korea Kusini pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushiriki kongamano la biashara na uwekezaji liliofanyika China Agost I6 mwaka huu kwa ajili ya kuhamasisha wawekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, amesema kuwa kupitia ziara ya kikazi aliyofanya mwezi huu nchini Korea kusini wamefanikiwa kuhamasisha wawekezaji na kuonesha nia ya kufanya uwekezaji.
Mwambe amesema kuwa akiwa korea ameshiriki kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika Agosti I3 mwaka huu ambapo wafanyabiashara walijadili fursa za uwekezaji katika sekta ya madawa na vifaa tiba.
Ameeleza kuwa katika ziara hiyo aliongozana na wawakikishi wa taasisi za serikali, Makapuni binafsi, Viongozi wa Chama Cha Watengenezaji na Wauzaji wa Madawa (TAPI) kwa ajili kupanua wigo wa Uwekezaji hapa nchini.
"Makongamano haya yaliambatana na ziara za kutembelea viwanda vinavyomilikiwa na baadhi ya makampuni ambayo yameonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania" amesema Mwambe.
Ameeleza kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo yamepatikana katika ziara hizo ni pamoja kusainiwa hati za maafikiano (MOU) tatu kati ya TAPI na wafanyakazi wa makampuni ya China ili kuwezesha mafanikio na makampuni ya Tanzania kuwekeza kwa ubia katika sekta ya Afya.
"Lengo la kushiriki magongamano hayo ni kuleta mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania" amesema Mwambe.
Katika hatua nyengine Mwambe amefafanua kuwa Kituo cha Uwekezaji kinaendelea kufanya kuboresha huduma za mahali pamoja (One stop facilitation Centre) ili kuwahudumia wawekezaji kwa ufanisi mkubwa.
Amesema kuwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na taasisi nyingine za serikali tayari wapo katika Ofisi TIC ili kutoa huduma kwa haraka hasa kwa wawekezaji wanaotoka nje ya nchi.
Katika kutengeneza Mazingira rafiki kwa wawekezaji taasisi zote zinafanya kazi kwa ukaribu na TIC ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafanikwa na kupiga hatua katika masula mbalimbali ya maendeleo.
USHINDI WA TIC KWENYE MAONESHO YA NANENANE, 20I8.
Ofisi za kanda za TIC zilishiriki maonesho ya wakulima (Nanenane) yaliyofanyika kikanda katika mikoa mbalimbali.
Katika maonyesho hayo TIC imefanikiwa kupata tuzo kutokana na utendaji bora Katika kazi zao.
Ofisi za TIC zilizofanikiwa kupata tuzo ni pamoja na Kanda ya Kusini (Mtwara) ambapo ilishika nafasi ya pili kwenye kundi la Taasisi za huduma na Utafiti.
Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam) na kanda ya Kati (Dodoma) kimefanikiwa kushika nafasi ya pili katika kundi la taasisi za kiuchumi na kufanikiwa kupata tuzo ya cheti.
Kutokana na uwepo za ofisi za kanda za TIC watanzania na wadau mbalimbali wanatakiwa kutumia Ofisi hizo katika kupata huduma mbalimbali.
MCHANGO WA TIC KATIKA KUWAJENGA WAJASIRIAMALI.
Mwambe amesema kuwa uwekezaji ndiyo njia sahihi ya kufikia uchumi wa viwanda jambo ambalo watahakikisha wanajenga sekta binafsi zilizo imara ili kufika mipango husika.
Amesema kuwa kituo kimejipanga kuwapa elimu wajasiriamali ili waweze kushiriki kutengeneza mifumo itakayowasaidia wazawa kukua na kuchukua nafasi ya uwekezaji hapa nchini.
"Msukumo wa TIC kwa sasa ni kuwaelimisha wajasiriamali wafanye shughuli zao za kiuchumi kwa ubunifu ili waweze kumudu mahitaji ya wawekezaji wakubwa" amesema Mwambe.
Ameeleza kuwa wanaendelea kuwapa hamasa wajasiriamali waweze kuzalisha bidhaa zao pamoja na kuhakikisha malighafi za kulisha viwanda zinapatikana ili kujenga uchumi wa Viwanda.
USHIRIKIANO WA TIC NA TAASISI ZA SERIKALI, SEKTA BINAFSI PAMOJA NA WANANCHI.
Mwambe amewataka viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali pamoja na sekta binafsi kuacha kuingilia majukumu ya taasisi nyengine kwa kutoa mtamko ambayo sio rafiki.
Amesema kuwa viongozi wakiwemo madiwani, wakuu wa walaya pamoja wakuu wa mikaoa wanaposhughulikia changamoto mbalimbali zinazohusiana na uwekezaji wanapaswa tutoa taarifa kwanza ili wapata ushauri jinsi kutatua matatizo.
"Ukiona kuna mwekezaji amefanya jambo ambalo sio rafiki ni vizuri mje TIC kutoa taarifa ili tuangalia namba bora ya kutatua changamoto" amesema Mwambe.

Post a Comment