Ads

KUMBILAMOTO AFUNGUA KAMPENI KWA KISHINDO , MAMIA WAJITOKEZA KUMUUNGA MKONO.

 Mwambawahabari
ALIYEKUWA Diwani wa Kata ya Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh:Omary Said Kumbilamoto, jana amefungua kampeni yake ya kwanza tangia ateuliwe na chama chake kipya cha CCM hii ni mara baada ya Kujihudhuru nyadhifa zake zote kuptia tiketi ya Chama cha CUF na kujiunga  Chama cha Mapinduzi (CCM ).

 Miongoni mwa Viongozi wa Juu wa Chama cha Mapinduzi waliohudhuria Ufunguzi huo wa Kampeni ni pamoja na  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Heri James ambaye alikuwa  Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa  CCM Mkoa wa Dar es Salaam ,Mh: Kate, Katibu Mwnezi wa CCM  Mkoa wa Dar es Salaam Mwakifamba , Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala ,Joyce Mkagaula, Bona Kaluwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga , na baadhi ya Makada wakubwa waliotoka Chama cha Upinzani CHADEMA wakiongozwa na Ndugu Mlaki na Viongozi wengine wa ngazi mbali mbali katika Mkoa wa Dar es Salaam na Wialaya zote.

Aidha katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Heri James, aliwataka Wakazi wa Vingunguti wasifanye makosa na kumchagua Omary Kumbilamoto ili azidi kuwatumikia wananchi wa Kata hiyo kwa kuwa Ilani ya CCM inatekelezeka ikiongozwa na Rais John Pombe Magufuli na wasaidizi wake katika ngazi mbali mbali.



Alisema kuwa wawapuuze wapinzania amabao kazi yao ni kupandikiza chuku dhidi ya Viongozi na Taiafa lao kwa Mabepari wa Ulaya jambo ambalo ni hatari sana na hawatalimezea mate  ili kuendelea kuimarisha nchi na Maendeleo kwa Wananchi wake waliyokiamini Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Wapinzani wao wanapinga kila jambo katika nchi hii, liwe zuri liwe baya , sasa wanatupa mashaka sana utasema wao si Watanzania kila jambo wanalipeleka  Ulaya, kwani Serikali yao haiwezi kuwasikiliza? Kiukweli lazima tukemee hili jambo na kamwe tusiwape madaraka watatupeleka motoni, tunahitaji Viongozi wenye busara na wachapa kazi kama ilivyo Kumbilamoto , hivyo wakazi wa Vingunguti tusifanye makosa siku ya kupiga kura tuhakikishe tunashinda kwa kishindo kikubwa na kumrudisha tena Kumbilamoto kuwa Diwani akawatumikie kiufasaha maana anajua shida zenu na mmetoka nae mbali sana”Alisema Heri James

Katika hatua nyingine, Mgombea kiti hicho cha Diwani, Mh: Kumbilamoto , aliwaeleza wakazi wa Vingunguti walichokivuna kipindi yupo Diwani na matarajio yake ya kuendeleza yale aliyoyaacha katika kuijenga Vingunguti Mpya.

Pia Kumbilamoto alisema kitu kilichompelekea kujihuzuru nyadhifa zake ndani ya CUF ni kutokana na Mgogoro unaoendelea ndani ya CUF pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Chama hicho kumshtumu kufanya kazi bega kwa began a Viongozi wa Serikali jambo ambalo kwa upande wake aliona halipo sawa.

“ Mimi ni mwanadamu najitambua, ili kufikia mafanikio ni lazima Viongozi wa Serikali wahusishwe kwakuwa wao wapo Madarakani , sasa wenzangu jambo hili hawalitaki kabisa, utaona maajabu kipindi tunapata Mafuriko Vingunguti hakuna hata Kiongozi mmoja wa CUF aliyejitokeza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wialya ya Ilala Dada yangu Sophia Mjema ndio walinisaidia, sasa kwa hali hii kweli utasema unabakia Kung’ang’ania  CUF, ndugu zangu naombeni mnipokee, kazi zangu mmeziona na nitazidi kuwasaidia bila ubaguzi wa aina yoyote kwa maslahi ya Wana Vingunguti”Alisema Kumbilamoto

Katika kuelekea tamati ya kufunga Kmapeni tulishuhudia baadhi ya Viongozi na makada wa Chama cha CUF wakijiunga na CCM wakimfuata Diwani wao wengi wao wakisema Chama chao kimekufa hivyo CCM ndiyo chama pekee chenye kutekeleza Sera zao kwa Vitendo.

Miongoni mwa wananchama waliorudisha kadi ni pamoja na Salma Emannuel, Mjumbe wa Kmati Tendaji ya Kata CUF, Adam Omary, Mwenyekiti wa Boda Boda upande wa CUF, Maulidi Mfunga Mwenyekiti wa Tawi la Mtambani tiketi ya CUF.

Kmapeni hizo zitaendelea tena kwenye Uwanja wa  Msikate

No comments