Ads

'' MAONYYESHO YA 42 YA BIASHARA SABASABA YAMETUNZUNZA MAMBO MENGI'' MANGULA




Mwamba wa habari
MAKAMU Mwenyekiti Chama cha Mapunduzi CCM Philip Mangula amesema uinguzwaji wa bidhaa kutoka nje unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara unaua soko la  bidhaa za ndani.

Pia amelipongeza Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF )Kwa kuwa washinda wa jumla katika maonyesho ya 42 ya biashara ya kimataifa na kuwataka kuhakikisha huduma zao zinaifikia Jamii nzima.

Akizungumza katika maonyesho hayo yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere sabasaba ambapo alisema bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zina ubora wa kutosha.

"Maonyesho haya yanatufunza mengi bidhaa za wenzetu zimeanza kutengenezwa miaka mingi sana  tukiziingiza hapa nchi tunalimaliza soko letu lakini niombe nimetembelea mabanda mengi wanafursa ya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma zao" alisema.

Alisema NSSF wanafanya juhudi kubwa katika kuwahudumia wananchi hivyo kutokana na utekelezaji wa Sera ya Ujenzi wa Uchumi kupitia viwanda ni vyema kujikita kutoa Elimu endelevu kwa wajasiriamali namna ya kunufaika na mikopo inayotolewa na shirika hilo.

"Mnajenga viwanda na mnatoa Mikopo kwa wajasiriamali wadogo naomba mhakikishe mnatoa elimu kwa wananchi namna watakavyonufaika na mikopo hii ili kujikwamua kiuchumi" alisema.







No comments