KIUNGO KUTOKA RWANDA ATUA NCHINI KUKAMILISHA DILI LA USAJILI SIMBA
Imeripotiwa kuwa kiungo mkabaji kutoka klabu ya Kiyovu SC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Rwanda, Fabrice Kakule, amewasili nchini kuja kufanya mazungumzo na Simba.
Kakule ametua nchini kufikia mwafaka na mabosi wa klabu hiyo ili kukamilisha dili la usajili tayari kuongeza makali katika safu ya kiungo kuelekea msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa.
Taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza kuwa mchakato wa kumpata mchezaji huyo umefanywa na Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, ambaye ametoa pendekezo la kikosi hicho kutafutiwa mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo.
Ujio wa kiungo huyo na dili lake likifanikiwa kukamilika, atakuwa anaungana na wachezaji wengine kama James Kotei, Jonas Mkude ambao wanacheza katika nafasi hiyo.
Ukiachana na Kakule, Simba pia wanahusishwa kuchukua saini ya Francis Kahata ambaye anakipiga Gor Mahia FCya Kenya ambaye yupo hapa nchini akishiriki mashindano ya CECAFA Kagame Cup

Post a Comment