Ads

KIGWANGALLA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA PORI LA AKIBA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla
MWAMBA WA HABARI.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amesimamisha kazi Meneja wa Pori la Akiba la Uwanda linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mark Chuwa kwa kushindwa kuondoa ng’ombe 12, 000 na wafugaji waliovamia pori hilo.
Pori la Uwanda liko katika Bonde la Ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa. Waziri Kigwangalla alichukua uamuzi huo baada ya kusomewa taarifa ya mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Halfany Haule akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangoba.
“Umeshindwa kazi (Chuwa ) kwa sababu una askari 26 na wewe mwenyewe lakini umeshindwa kuwaondoa ng’ombe 12,000 na wafugaji waliovamia na kuchunga katika Pori Akiba la Uwanda .... Lakini bado mnalipwa mshahara bila kutimiza wajibu wako au umelipwa fedha nina taarifa ya kuwa mnapokea rushwa.
Kuanzia sasa nakusimamisha kazi nataka maelezo ya kutosha,” alisema. Awali akisoma taarifa ya mkoa, Dk Haule alimweleza Waziri Kigwangalla kuwa ng’ombe wapatao 40,000 waliingia na kuchungwa ndani ya Pori la Akiba la Uwanda ambapo baada ya kuondolewa kwa nguvu wamebakia ng’ombe wapatao 12,000. Dk Kigwangalla yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne aliyoianza jana mkoani Rukwa. Chanzo; habari leo.

No comments