KAMPUNI YA TMRC YAORODHESHWA HATIFUNGANI BILIONI 120 DSE.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Ashatu Kijaji akiwa (katikati ) akizungumza jambo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuorodhesha hatifungani za kampuni ya TMRC katika soko la hisa (DSE).
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Kampuni ya mikopo ya nyumba (TMRC) imefanikiwa kuorodheshwa hatifungani
yenye thamani ya bilioni I20 katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) jambo
ambalo litasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia
fursa zilizopo katika sekta ya masoko katika mitaji.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuorodhesha hatifungani za kampuni ya TMRC soko la hisa (DSE) Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa hatua ya TMRC ni
mkakati wa maksudi wa kutekeleza jukumu lake la msingi la kutafuta na kukuza
mtaji kwa ajili ya kuinua sekta ya mikopo ya nyumba pamoja na mitaji.
"Hatifungani ya
TMRC ni ya muda wa miaka mitano ambayo kitaalamu itaipatia kampuni fedha za kukopesha
mabenki kwa ajili ya mikopo ya nyumba kwenye soko la fedha za ndani"
amesema Dkt. Kijaji.
Amesema hatua hiyo itachangia kukua kwa
masoko ya mitaji hapa nchini, kwani ni wakati mwafaka sekta ya fedha
kuwa imara kwa kuendelea kuchachua ukuaji wa uchumi.
Dkt. Kijaji ameeleza kuwa kampuni ya TMRC katika utendaji wake imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shillingi bilioni 91 kwa Benki I4 hapa nchini, huku watanzania 937 wakinufaika moja kwa moja na mikopo itolewayo.
Amesema wananchi 4,209 wamenufaika na mikopo ya nyumba kutokana na uwepo wa mfumo wa mikopo ya nyumba unaowezeshwa na TMRC.
''Katika
kuhakikisha mikopo ya nyumba inaanzishwa serikali kwa kushirikiana na
Benki ya dunia ilianzisha mradi wa kuwezesha kuwepo kwa mfumo wa mikopo ya
nyumba (Housing Finance)'' amesema Dkt. Kijaji
Amefafanua kuwa katika kusaidia upatikanaji
wa mikopo ya nyumba kwa gharama nafuu kwa kutumia teknolojia mbadala, mashirika
kadhaa yamehusishwa ikiwemo shirika la nyumba la taifa (NHC), Shirika la Utafiti wa Ujenzi (NHBRA) pamoja na Watumishi Housing (WHC).
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya
Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama, ameipongeza
bodi ya uongozi wa kampuni ya TMRC kwa kufanikisha uorodheshaji wa hatifungani
ya katika soko la hisa.
Amesema kuwa kazi waliofanya haikuwa ndogo
na rahisi kwani wamefanya kwa uweledi na kwa ufanisi mkubwa.
"Fedha zipatikanazo kupitia mauzo ya
hatifungani zitatumika kugharamia shughuli za maendeleo ya kampuni ya TMRC
pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa benki zinazotoa mikopo ya
nyumba" amesema Mkama.
Mkama ameeleza kuwa kupitia hatifungani
hiyo Kampuni itakuwa na uwezo mkubwa wa kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali
ya maendeleo katika kukuza sekta ya nyumba kufuatana na mpango wa biashara wa
TMRC.
"Taasisi za fedha, bima na Kampuni
zingine kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ili kupata
fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo" amesema Mkama.
Ametoa rai kwa wadau wa masoko
ya mitaji kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza mipango ya
kuendeleza mitaji ikiwemo kuleta bidhaa mpya ambazo zitaorodheshwa katika soko
la hisa.
Kuorodheshwa kwa hatifungani katika soka la
hisa ninakuwa ni jambo kubwa katika maendeleo ya masoko ya mitaji hapa nchini
pamoja na ukanda wa afrika Mashariki, kwani kamapuni ya TMRC inakuwa ni
hatifungani ya kwanza yenye muundo wa kudhaminiwa na mali (Asset Backed
Security-ABS).
Post a Comment