Croatia Yaitandika England 2-1 Na Kufanikiwa Kuingia Fainali Kombe la Dunia
Mwamba wa habari

Timu
ya Taifa ya England imeaga michuano ya Kombe la Dunia kwa kupoteza
mchezo wa nusu fainali dhidi ya Croatia kwa idadi ya mabao 2-1.
Katika
mchezo huo, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1
na kuamuliwa kuongezwa dakika30 za ziada ili kupata mshindi wa mechi.
England
walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 5 ya mchezo kwa njia ya
mpira wa adhabu uliopigwa na kuwekwa kimiani na Kieran Trippier na
baadaye kipindi cha pili Croatia walisawazisha kupitia kwa Ivan Perisic
dakika ya 68.
Baada
ya dakika 90 kumalizika kwa sare hiyo, 30 zingine ziliongezwa na
Croatia walizitumia vema kwa straika wake, Mario Mandzukic kuandika bao
la pili kwenye dakika ya 106.
Mpaka Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo yalibaki kuwa 2 kwa Croatia na 1 kwa England.
Kutokana
na England kuondoshwa , sasa itacheza dhidi ya Ubelgiji kusaka mshindi
wa tatu Jumamosi huku Croatia ikiungana na Ufaransa kucheza fainali
Jumapili ya wiki hii.
Post a Comment