BUNGE LAPITISHA SHERIA TATA KUBANA MITANDAO YA KIJAMII
Rais Abdel- Fattah el- Sissi
Bunge la Misri limepitisha sheria tata inayolenga kudhibiti mitandao maarufu ya kijamii inayochapisha habari za uongo.
Mswada huo uliopitishwa Jumatatu wiki
hii unaliwezesha bunge kuzuia akaunti binafsi ya mtu katika mitandao ya
kijamii iliyo na wafuasi zaidi ya 5,000 kutokana na kuchapisha taarifa
za uongo.
Hata hivyo muswada huo lazima usainiwe na Rais Abdel- Fattah el- Sissi ili uwe sheria.
Chini ya utawala wa el-Sissi Misri
imewatia mabaroni , kuwashitaki na kuwafunga waandishi wa habari
kutokana na makosa ya mitandao ya kijamii.
Iwapo muswada huo uatasainiwa kuwa
sheria baraza la juu la habari nchini humo litasimamia akaunti maarufu
katika mitandao ya kijamiii zitakazokuwa zikiendeshwe kama vyombo vya
habari.
Waandishi wa habari wasio na mipaka
waliitaja Misri kuwa ya 161 kati ya nchi 181 kwenye orodha yake ya mwaka
2017 ya Uhuru wa vyombo vya habar
Post a Comment