Wahasibu, Waweka Hazina Watakiwa Kutumia TEHAMA Kusimamia Fedha za Maendeleo
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili kwa waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi na Mbeya wakati akifungua awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.
Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka mradi wa uimarishaji mifumo katika sekta za umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa akitoa maelezo ya awali kuhusu faida za mifumo mbalimbali iliyojengwa na Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na PS3 ili kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi katika mamlaka za Serikali za Mitaa, mafunzo hayo waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe , Katavi na Mbeya wakati wa hafla ya kufungua awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.
Sehemu ya waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe , Katavi na Mbeya wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali wakati wa hafla ya kufungua awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.
Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma Bw. Onesmo Raphael ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mafunzo ya siku nne kuhusu matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kwa waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe , Katavi na Mbeya akimkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo yanafanyika jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali (kulia) akifurahia jambo na Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka mradi wa uimarishaji mifumo katika sekta za umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa mara baada ya hafla ya ufunguzi wa mafunzo kwa waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe , Katavi , awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya. Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo ya wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi, awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo kama wanavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akisisitiza jambo kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi, awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

Mweka hazina wa halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Bw. Mabula Mponeja akisisitiza jambo wakati wa mafunzo kwa wahasibu
na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi, awamu ya pili ya
mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya)
Na: Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya
Serikali imewaagiza Wahasibu na Waweka Hazina kusimamia
kikamilifu fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika
Halmashauri zao kote nchini kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) iliyopo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TEHEMA kutoka Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Bw. Erick
Kitali, wakati akifungua awamu ya pili ya mafunzo ya siku nne kuhusu
matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa
ya Njombe, Songwe, Katavi na Mbeya. Mafunzo hayo yanafanyika jijini
Mbeya ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau
wa maendeleo kuimarisha mifumo ili kuongeza tija katika huduma zinazotolewa
kwa wananchi.
“Kama mweka hazina au mhasibu lazima uwe mstari
wa mbele kuhakikisha kuwa kila eneo ambalo kuna fedha za Serikali mnazisimamia
kikamilifu kwakuwa hakuna atakayevumiliwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu
yake vyema kwa kutumia mifumo hii ambayo imeimarishwa kwa maslahi ya
Taifa,” alisisitiza Kitali.
Mfumo wa Epicor 10.2 uko chini ya Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), na umejengwa
kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi huu wa miaka mitano unatekelezwa
katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
Akifafanua, Bw. Kitali amesema kuwa washiriki
wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa la kuelewa matumizi ya mfumo wa Epicor
10.2 kwa ufasaha katika kipindi chote cha mafunzo, ili kuepuka kutekeleza
majukumu yao kinyume na taratibu za mifumo hii ambayo kwa sasa imeunganishwa
na kuweza kuongea ili kurahisisha utendaji na kuchochea maendeleo endelevu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka Mradi
wa PS3, Bw. Desderi Wengaa, amesema kuwa OR-TAMISEMI imekuwa ikifanya
kazi kubwa kwa kushirikiana na mradi huo katika kuimarisha mifumo ikiwemo
wa Epicor 10.2.
Aliongeza kuwa mifumo yote sasa imeunganishwa hadi
ngazi ya watoa huduma, hali inayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma
kwa wananchi na hivyo kusaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji katika
ngazi za vituo vya kutolea huduma.
Kutokana na kuimarishwa kwa mifumo hiyo, Serikali
imeweza kuongeza ukusanyaji wa mapato na huduma zinazotolewa kwa wananchi
katika vituo vya kutolea huduma zikiwemo za afya na elimu.
Akizungumzia lengo la mafunzo ya matumizi ya mfumo
wa Epicor 10.2, Bw. Wengaa alieleza kwamba ni kuwajengea uwezo wahasibu
na waweka hazina kusimamia rasilimali fedha kikamilifu katika maeneo
yao ili dhamira ya Serikali kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma bora
itimie.
Mafunzo hayo yanayoendeshwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana
na Mradi wa PS3, yameingia katika awamu ya tatu wiki hii, baada ya awamu
ya kwanza nay a pili kufanyika wiki iliyopita. Licha ya Mbeya,
mfunzo kama haya yanayohusisha washiriki kutoka nchi nzima yanaendelea
pia katika vituo vingine, ambavyo ni mikoa ya Iringa, Dodoma, Mwanza,
Mtwara na Kagera.
Post a Comment