Ads

Team King Kiba, Samatta kuvaana Jumamosi kuchangia elimu



Mwamba wa habari
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba 'King Kiba' na Mcheazji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk, Mbwana Ally Samatta wanatarajia kucheza mechi Juni 9 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lengo likiwa kuchangia fedha za kusaidia wanafunzi wa Shule za Msingi nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Msanii huyo wakati akizungumzia mchezo huo utakaowakutanisha wachezaji wa kimataifa wanaocheza klabu mbalimbali nchini.

Amesema fedha zitakazopatikana zitakwenda kuchangia miundo ya elimu katika shule hizo za msingi kwamba mchezo huo upo chini ya Kampeni iliyopewa jina la Nifuate.

" Mimi na Samatta tumeplan jambo la msingi tumeonelea tuandae mchezo huo kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaosoma shule za msingi hatuataishia Dar es Salaam programu hii ni endelevu," amesema.

Amebainisha kuwa yeye atatunda timu yake na Samatta atachagua wachezaji wake na kwamba tayari Mchezaji anayekipiga nchini Afrika Kusini amekubali kuungana na timu yake.

Amewataka wananchi na wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kufanikisha upatikanaji wa fedha utakaosaidia watoto kupata elimu katika mazingira rafiki.

Kwa upande Meneja Msimamizi wa Kampuni ya ASAS, Fahad Ally amesesma kampuni hiyo imeamua kujitosa katika kudhamini mchezo huo kwa ina kawaida kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo ya hivi karibuni ya kuwapa maziwa wanafunzi wa shule hizo mkoani Iringa.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii inayohitajika nchini.

No comments