TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan akiwa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Januari Makamba wakikagua mabanda leo katika maadhimisho ya mazingira duniani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kwenye uhitimishwaji wa siku ya mazingira (Picha zote na Noel Rukanuga)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluh Hasan amewataka viongozi na taasisi kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika uharibifu wa mazingira.
Akizungumza leo katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani Makamu wa Rais Samia amesema kuwa ni muhimu wananchi wakachukua hatua katika
kuhakikisha wanayatunza mazingira na hivyo serikali imeweka mikakati ya
kukabiliana na waharibifu wa mazingira.
Awali akizungumza Waziri
wa nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Januari Makamba, amesema watahakikisha wanaendeleza jitihada za kuyahifadhi mazingira kwa kuwapa
elimu wananchi watumie nishati mbadala na kuepuka mayumizi ya mkaa.
Alvaro Rodrigues ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa akiwa
amehudhuria kwenye maadhimisho hayo amesema watahakikisha wanaendelea kufanya
kazi kwa pamoja na wananchi wote katika kuyatunza mazingira.
Kwa upunnde wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema kuwa kuanzia leo ametangaza oparesheni kabambe ya kuwakamata na kuwatoza faini wachafuzi wa Mazingira.
Amesema kuwa lengo la kuhakikisha jiji linakuwa kwenye hali ya usafi kama majiji mengine ulimwenguni.
RC Makonda amesema kuwa ameandaa vijana zaidi ya 4,000 kutoka Jeshi la kujenga Taifa JKT ambao watafanya kazi ya kuwakamata watupaji wa taka barabarani na mitaani.
"Vijana hao 4,000 ni wale waliomaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi " amesema RC Makonda.
Ameeleza kuwa faini itakayopatikana kwa wachafuzi, vijana watachukua 40% na 60% itaingizwa serikalini.
RC Makonda amesema hawezi kukubali kuona jiji linakuwa kwenye hali ya uchafu wakati ipo na sheria ya mwaka 2004 inayotoa mamlaka ya kuwawajibisha wananchi wenye tabia kuchafua mazingira kwa makusudi.
Amesema kuwa itakumbukwa kila mwaka viongozi wamekuwa wakihimiza usafi na hata alipokuja Rais Barack Obama miaka kadhaa iliyopita barabara zilipigwa deki na alipoondoka uchafu ukaendelea.
RC Makonda ameamua sasa kuja na mkakati wa kuwatumia vijana wa JKT wasiokuwa na kazi kufanya jukumu la kuwakamata wachafuzi wa mazingira.
Post a Comment