Ads

Samia awataka wana Dar es Salaam kutunza miundo mbinu ya Ukuta Wa Barabara ya Barrack Obama.


Hussein Ndubikile 
Mwambawahabari
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuitunza  na kuhifandhi miundo mbinu  ya Ukuta uliopo Barabara ya Barack Obama huku akibainisha ikitunzwa na kuhifadhiwa itadumu zaidi ya miaka 70.

Aidha, amewaomba viongozi wa dini kusaidia kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira yao.
Wito huo ameutoa leo jijini humo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani wakati akizindua Ujenzi wa ukuta huo uliofadhiliwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP).

Amesema wananchi watakaotumia ukuta huo wanatakiwa kutambua umuhimu wa kuutunza na kuujali kwa kuhakikisha miundo mbinu iliyowekwa inadumu kwa muda mrefu.

“ Mtakaotumia ukuta huu msiharibu miundo yake muhakikishe mazingira yake yanatunzwa na kuhifadhiwa kikamilifu,” amesema.

Amebainisha kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira yakiwemo mafuriko yanayosababishia S            erikali hasara ambapo mwaka 2011 ilitumia Sh bilioni 4.5 kugharamia miundo mbinu iliyoharibiwa na mafuriko.

Amesisitiza kuwa lengo la kujenga ukuta huo ni kuzikinga kingo zilizopo karibu na barabara hiyo zisiliwe na maji ya baharini.

Amefafanua kuwa ukuta kama huo pia umejengwa Pangani- Tanga na Kilimani-Zanzibar na kwamba utakapokamlika utakabidhiwa kwa Halamshauri ya Jiji
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais, Muungano na Maziungira, January Makamba amesema ukuta huo una urefu wa mita 920 na kusisitiza ukitunzwa utadumu muda mrefu.

Katika hatua nyingine Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan akiwa katika kiliele cha maadhimisho hayo kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja ameitaka jamii kuacha tabia ya kukata miti hovyo badala itunze na kuyahifadhi mazingira kwa masilahi ya vizazi vilivyopo na vijacho.

Pia amesema kukata miti hovyo husababisha uoto wa matunda ya asili kupotea, makazi ya wadudu ya wanaofanya shughuli za Ekolojia kuharibika, kushindwa kwa unayonyaji wa hewa ukaa pamoja na ukosefu wa dawa za asili zitokanazo na misitu assili.

Ameezitaka taasisi za kiaraia Mashirika binafsi kusimamia ipasavyo Sheria na Kanuni za Uhifadhi mazingira.

 Mratibu Mkazi Wa Umoja Wa Mataifa Nchini, Alvaro Rodriguez ameipongeza Serikali kwa juhudi za dhati za utunzaji na uhifadhi wa mazingira. 



Alvaro amesema nchi nyingi zinakabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na uharibifu wa mazingira na kusisitiza juhudi zinafanywa kwa pamoja kukabiliana na changamoto hiyo

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul amesema ifikapo Julai Mosi Mwaka huu kutaendesha Oparesheni kabambe ya usafi lengo ni kuhakikisha mazingira ya mkoa huo yanakuwa safi.

No comments