RAIS DKT. MAGUFULI KUZINDUA ASDP II JUNE 4 MWAKA HUU
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt Charles Tizebe akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam.
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wizara za kisekta zinatarajia kufanya uzinduzi wa program ya kuendelea sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II) inayotarajia kufanyika June 4 mwaka huu jijini Dar es Salaaam, huku mgeni rasmi akitarajia kuwa Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Wizara hizo za kisekta ni Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Viwanda Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Umwagiliaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt Charles Tizebe, amesema kuwa programu hiyo itatekelezwa katika Mikoa na Wilaya zote kwa kuzingatia mazao ya kipaombele kufuatana na ikolojia ya Kilimo ya kanda kwa miaka 10 kwa vipindi vya miaka mitano mitano.
Amesema kuwa katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wa programu Utaanza mwaka 20I8/I9 hadi 2023/24
"Lengo la programu hii ni kuleta mageuzi katika sekta ya Kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na kuongeza pato la wakulima, wafugaji na wavuvi" amesema Mhe. Dkt Tizeba.
Dk Tizeba ameeleza kuwa programu hiyo itatekeleza sera mbalimbali za kitafia ikiwemo Sera ya Kilimo ya taifa, Sera ya mifugo ya Taifa, Sera ya Uvuvi, Sera ya Masoko ya Mazao, Sera ya Ugatuaji madaraka, Sera ya Umwagiliaji ya Taifa, Sera ya Usalama wa chakula na Lishe.
Amesema kuwa pia kuna sera ya maendeleo ya Ushirika, Sera ya Mashirikiano kati ya sekta za Umma pamoja na sekta binafsi.
"Washiriki katika kufanikisha programu hii ni wadau wa sekta ya kilimo , mifugo, uvuvi, Ushirika, Wizara, Taasisi za serikali na zisizo za serikali, Washiriki wa maendeleo, sekta binafsi pamoja na wadau wote" amesema Mhe. Tizeba.
Post a Comment