Ads

Jumuiya ya Wazazi Ilala kushirikiana na serikali kutunza Mazingira



Na Heri  Shaaban
Mwambawahabari
JUMUIYA ya Wazazi WILAYA ya ILALA imesema itashirikiana na serikali katika utunzaji mazingira.

Hayo yalisemwa na Katibu wa ELIMU ,malezi na Mazingira Wilaya ya Ilala Wilson Tobola wakati wa wiki ya Mazingira viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Wilison alisema wao kama jumuiya ya Wazazi Ilala wanashirikiana na Serikali katika kupanda miti katika wilaya ya Ilala na kutunza Mazingira.

"Nazungumza kwaniaba  ya viongozi wangu wa jumuiya hii ya Wazazi WILAYA ya ILALA  tutashirikiana na serikali katika utunzaji wa mazingira na kuakikisha mazingira ya Ilala yanakuwa na miti ya kutosha"alisema Wilison.

Alisema kila Mwananchi wa Ilala ana wajibu wa kupanda miti na Kitunza mazingira ya eneo lake..

Aliwataka wananchi kutunza mazingira yao na kuifadhi Takataka katika kifaa ama chombo malum bila  kuleta uchafuzi katika mazingira yao.

Alitoa wito kwa wakazi wa Ilala Kitunza mazingira na kupanda miti na kuakikisha Maeneo yote yanakuwa safi kuepuka magonjwa ya mlipuko .


Alisema moja ya jukumu la jumuiya hiyo kusimamia utunzaji wa mazingira na miti mingi WA wameweza kupanda katika wilaya hiyo katika baadhi ya Kata.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA aliwataka wananchi kushirikiana serikali katika utunzaji wa mazingira.

SOPHIA MJEMA alisema katika wiki ya mazingira WILAYA yake imekuwa mwenyeji kitaifa madhimisho hayo wanazimisha kwa kushiriki kwa vitendo katika maonesho mbalimbali sambamba na makongamano juu ya utoaji ELIMU ya Mazingira na upandaji miti.

Alisema katika wilaya ya Ilala waliweka malengo ya ngo ya upandaji miti milioni moja na kampeni hiyo imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa upandaji miti kila Kata. 





No comments