OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZO KWA WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari, akizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa wanafunzi Kidato cha Nne na cha Tano waliofanya vizuri kitaifa katika masomo ya Baioloji na Kemia iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Esther Hellen Jason akizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kutoa zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi, Kemia na Baioloji
Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa katika masomo ya kemia na bailojia katika kipindi cha mwaka 2016 na 2017.
MWAMBA WA HAABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita pamoja na walimu wamefanikiwa kupewa tuzo na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kufanya vizuri kitaifa katika Masomo ya kemia na Baiolojia mwaka 20I6 na 20I7.
Tuzo hizo ni vyeti pamoja na fedha ambapo mshindi wa kwanza hadi watatu kwa kidato cha nne amepewa 450,000/=, 400,000/=, 350,000/=.
Kwa kidato cha sita mshindi wa kwanza amepata 500,000/=, pili 400,000/=, tatu 350,000/=, huku upande wa walimu wamepewa 500,000/= kila mmoja.
Akizungumza katika hafla fupi ya kugawa tuzo hizo Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi, amesema kuwa masomo ya bailojia na kemia ni muhimu katika kufanikisha maendeleo hapa nchini.
Amesema kuwa masomo hayo ni muhimu, kwani watu wanaosoma masoma hayo wapo katika soko la ajira tofauti na masomo mengine.
"Taaluma ya masomo ya kemia na bailogia imekuwa ikizalisha wataalamu wengi hapa nchini ambao wamekuwa na manufaa kwa taifa" amesema Prof Kambi.
Prof Kambi ambaye alikuwa anamwakilisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile , amefafanua kuwa changamoto iliyokuwepo ni wanafunzi kutopenda masomo ya sayansi.
Amesema kuwa wanafunzi wengi wanasoma masomo ambayo yanazalisha wataalamu katika soko la ajira tayari wamezidi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Esther Hellen Jason, amesema kuwa utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya kemia na bailojia ni mwendelezo, kwani walianza utaratibu huo tangu mwaka 2007.
Amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kutoa tuzo hizo kwa wanafunzi I68 pamoja na walimu I2 ambao wamefanya vizuri.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko, amesema kuwa lengo la kutoa tuzo hizo ni kuleta hamasa ya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kupenda masomo ya sayansi jambo ambalo litasaidia katika soko la ajira pamoja na kuwa wataalamu wa masuala mbalimbali.
"Tunatoa tuzo hizi ili kuwapongeza na kuleta hamasa katika kuyapenda masomo ya sayansi " amesema Mafumiko.
Mwanafunzi wa sekondari ya Kibaha ambaye ameshika nafasi ya pili kitaifa kwa somo la kemia huku bailojia akiwa nafasi ya tatu, Paschal Joseph, ameeleza kuwa kupenda masomo hayo na kusoma kwa bidii ni miongoni mwa vitu vilivyosaidia kufanya vizuri.
Joseph ambaye amefanya vizuri masomo hayo kwa kidato cha nne mwaka 20I6, amesema kuwa ili uweze kufanya vizuri zaidi jitiada binafsi zinaitajika.
Wanafunzi walipewa tuzo na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kidato cha sita ni pamoja na Agatha Ninga-Tabora Girls, Sophia Juma-St. Mary'S, Doreen Smart- Waja Girls.
Wavulana ni Nathanael Ndagiwe-Mzumbe, Shabani Kaniki- Majengo, Benedict Msangi- Mzumbe.
Kwa kidato cha nne ni Samaiya Mussa-Zanzibar Fedha, Amira Moh'danad- Fidel Catro, Nelda John- Marian Girls, Abuubakar Ali Hassan- Fidel Castrol, Pascal Joseph-Kibaha, Benjamini Herman- Pugu.
Wengine ni Nelda John- Marian Girls, Irene Ambrose Gerald- Kifungilo Girls pamoja na Christa Kobulungo Eduward kutoka St. Francis Girls.
Post a Comment