Ads

MWANAMKE AUAWA , AMEZWA NA CHATU.


File photo - Close up of a Reticulated Python headHaki miliki ya AGES
Image caption

MWAMBA WA HABARI
Mwanamke mmoja nchini Indonesia ameuawa na kumezwa mzima mzima na chatu mwenye urefu wa mita 7.
Licha ya visa kama hivyo kuwa vichache hiki ndicho kisa ya hivi karibui cha mtu kuuliwa na chatu nchini Indonesia kwa takriban mwaka mmoja.

Ni kipi kilimpata mwanamke huyo?

Wa Tiba, 54, alitoweka Alhamisi iliyopita wakati akiwa kwenye shamba lake la mboga katika kisiwa cha Muna mkoa wa Sulawesi. Shughuli kubwa ya kumtafuta ilifanywa na wakaazi wa eneo hilo.
Viatu vyake na upanga vilipatikana siku moja baadaye huku chatu aliye na tumbo limefura akipatikana mita 30 kutoka eneo hilo.
Wenyeji walishuku kuwa nyoka huyo alimuua, kwa hivyo wakamuua na kumtoa shambani.
Tumbo la nyoka huyo lilipasuliwa na mwili wa mwanamke huyo ukapatikana ndani.
Picha za kutisha zimekuwa zimekisambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Indonesiaa zikionysha mwili wa mwakame huyo ukitolewa tumboni mwa chatu huyo mbele ya umati mkubwa.
Chatu wanashambuaje?
Chatu wa sulawesi wanaweza kukua hadi urefu wa miaa 10 na wana nguvu sana, Wanashambulia kwa kuvizia, wakijifungia kwa windo lao na kulivunja kwa kufinya hadi kuua.

A Reticulated Python belongs to Steven Prasetyo is seen in Jakarta, Indonesia on January 23, 2018.Haki miliki ya picha
Image captionReticulated pythons are usually said to avoid humans

Wanaua kwa kuzuia windo kupumua na kwa mshutuko wa moyo kwa dakika chache
Wakati inapowadia kuwala binadamu, kizuia huwa na mabega ambayo hayawezi kuvunjika. Mary-Ruth Low mtunzaji wa mbuga za wanyamapori huko Singapore ni mtaalamu wa chatu aliambia BBC.

Wanakula wanyama wakubwa?

Kawaida chatu hula panya na wanyama wengine wadogo, lakini mara wanapofikia ukubwa fulani hukosa hamu ya kula panya tena kwa sababu ni wadogo sana.
Sasa wao huanza kuwalenga wanyama wakubwa kama nguruwe au hata ng'ombe.

Image of a man cutting open a huge snake with a long knife, while villagers look on. Salubiro village, Karossa, Central Mamuju, West Sulawesi, Indonesia. Published by Tribun Timur on 28 March 2017.Haki miliki ya pich
Image caption

Mwaka uliopita mwanamume mmoja kwenye mkoa wa Sumatra nchin Indonesia alifanikiwa kumshinda nguvu chatu mwenye urefu wa mita 7.8 ambaye alikuwa amemshambulia kwenyw shamba lake. alinusurika na majeraha mabaya. chanzo Bbc 

No comments