Ads

DC MJEMA AZINDUA RASMI KAMBI YA WAREMBO ILALA , ATAMBA MISS TANZANIA ATATOKA ILALA.

 

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Miss Ilala  2018 wakiwa katika kambi ya kujiandaa na mashindano katika Hotel ya Lamada Ilala jijini Dar es salaam.


Mwamba wa habari 
 Na.John Luhende
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mhe Sophia Mjema amewataka wasichana wanaoshiriki mashindano ya miss Ilala 2018, kujiamini na kuwa wabunifu na kushiriki katika shughuli za maendeleo katikajamii.


Mhe Mjema Ameyasema hayo katika hotel ya Lamada Ilala wakati akizindua rasmi kambi ya kujiandaa na mashindano ya Miss Ilala  yanayotarajiwa kufanyika Julai 6/2018, na kuahidi kuwa ofisi yake itafanya  kazi kwa kushirikiana na washiriki wote katika shughuli za kijamii na kuhamasisha maendeleo.


Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Miss Ilala  2018 wakiwa katika kambi ya kujiandaa na mashindano katika Hotel ya Lamada Ilala jijini Dar es salaam.


"Napenda niwatie moyo kuwa ninyi ni wasichana warembo na mtafika mbali na mshindi wa Miss Tanzania atatoka Ilala kwakuwa nimewaona mnaweza" alisema


Aidha Mjema Manispaa ya Ilala itagharamia zawadi za washindi , ametaja zawadi za mshindi na washiriki za washiriki wa mashindano hayo kuwa, mshindi wa kwanza atapewa Kiwanja na hati.
Mshindi wa pili milioni. Moja na eneo la biashara.wa tatu anapelekwa chuo chaurembo kusoma miezi sita, wa nne atapewa Dina siku mbili five star hotel.wa tano atazawadiwa Dryer ya  Saloon.

"Katika mashindano  Kuna namba ya kwanza ya pili na kuendelea  sasa wotowangu  hujashinda usinune , wewe katika kuingia katika kambi hii tayari sisi tumeshajenga kuona utafanya kazi na sisi kwa muda wa mwakammoja" alisema 

Kwa upande wake mlezi wa wasichana hao  Diwani wa Vingunguti ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amemshukuru DC Mjema kwa Wilaya yake kujitoea kutoa zawadi za washindi wa mashindano hayo  na kuahidi kuwa mashindano hayo yatafanyika  kwa haki na  nayeye kama mlezi atakuwa karibu na walimbwende hao kuhakikisha wanapewa mafunzo  yanayostahiki ili waweze kupata  mshindi bora.

No comments