Ads

DC Ilala kushirikiana na TAMWA kutokomeza ukatili


Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
MKUU wa Ilala Sophia Mjema amesema atashirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA )katika kupinga ukatili katika wilaya ya Ilala.


Sophia Mjema aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ilioandaliwa na TAMWA.


"Kama mkuu wa Wilaya  hii tutapinga ukatili kwa kushirikiana na TAMWA  ndani ya wilaya yangu sitafumbia macho vitendo hivyo "alisema Mjema.

Alisema mikakati yake katika wilaya hiyo kujenga hosteli katika shule zote Ilala ili wanafunzi wapate mda wa kujisomea .

Alisema atazungumza na Mkurugenzi wa Ilala ili kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa hostel za wanafunzi kwa Ilala inawezekana .

Alisema awali alikuwa mkuu wa wilaya Rushoto mpango wa kujenga nyumba za wanafunzi shuleni ulifanikiwa hivyo na ILALA lazima mpango huo ufanikiwe.


Aidha  alisema pia marufuku kwa Wanafunzi Ilala kushika mimba wakati yupo masomoni.


Aliwataka Wazazi kuendeleza watoto  katika elimu ili kuongeza ufaulu katika wilaya ya Ilala.

Alisema taasisi za kiraia hususani TAMWA zinazochangia azima na juhudi za Serikali kuhakisha watoto wetu wanalindwa dhidi ya ukatili wa aina Zote na kutimiziwa haki yao ya MSINGI ya kupata elimu.

Mjema alisema chama cha waandishi wa habari Wanawake TAMWA kinatetea haki za Watoto wa kike kiasi cha kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika


Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAMWA Edda Sanga alisema TAMWA imekuwa ikichangia juhudi za serikali katika kuboresha haki na USTAWI wa watoto hapa Tanzania kupitia shughuli zake za uchembuzi kwenye vyombo vya Habari  ,kwenye Jamii na Katika Shule ili kupunguza changamoto nyingi ambazo watoto wanakutana nazo kama mimba za utotoni., unyanyasaji wa kijinsia, dhuluma katika mirathi .

No comments