WANUFAIKA MIRADI YA TASAF MANISPAA YA ILALA WATAKIWA KUITUNZA NA KUIENDELEZA MIRADI.
Na.John Luhende.
mwamba wa habari
Afisa Tawala Wilaya ya Ilala Jabiri Omary Makame ,akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Ilala amewataka wanufaika wa miradi ya TASAF katika mtaa wa Mtambani ‘B’ kuitunza miti waliyopanda katika mradi unaotekelezwa na Mpango wa Taifa wa kunusuru kaya masikini ili waweze kupata miradi mingine.
Aidha, amewapongeza Wananchi hao kwa kuendeleza kwa mafanikio mradi wa upandaji miti katika mitaa ya kata yao. Mradi huu wa TASAF ulianzishwa na Serikali ili kuzikwamua kiuchumi kaya masikini,
Akizungumzia changamoto za uwepo wa garage (Gereji) za Magari katika maeneo yao, ameagiza Uongozi wa mtaa kuandaa taarifa na kuipatia ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kwamba changamoto zote walizo zisema ofisi itazifanyia kazi ili Wananchi hao waweze kujiendeleza kiuchumi.
Amewataka Viongozi wa TASAF katika miradi ijayo kuupa kipaumbele mtaa wa Mtambani ‘B’ kwakuwa wamefanya vizuri katika mradi uliopita.
Hata hivyo ameitaka TASAF Wilayani Ilala kuvipa kipaumbele vikundi vilivyotekeleza kwa mafanikio miradi yote katika awamu zilizo pita katika mtaa wa mtambani ‘B’.
‘’Nimefurahishwa na taarifa yenu kusema kuwa mmetekeleza kwa mafaniko makubwa mradi wa uhifadhi mazingira kwa kupanda miti, ninyi ni Watu wenye moyo na ari kubwa na Mimi nawomba TASAF muwape kipaumbele na pia naomba hii miti muitunze hadi ikue’’. Amesema
Kwa upandewake kaimu mratibu miradi TASAF Manispaa ya Ilala Ester Kaboma ameeleza mradi huo wa ajira za muda umelenga zaidi katika kuwasadia walengwa kujipatia kipato na mradi huu umetekelezwa kwa awamu tatu na mlengwa akishiriki mradi huo atajipatia jumla ya shilingi 34500 kwa siku 15 kwa muda wa saa nne na kuongeza kipato katika Ruzuku yake ya kawaida ambayo anapokea.
Amesema Manispaa hiyo imepokea jumla ya shilingi 207 milioni sawa na 75 % kwaajili ya ujira wa walengwa wa TASAF katika mitaa kwa malipo ya Disemba 2017 na January 2018,pia wamepokea asilimia 25% kiasi cha shilingi 51,380000 kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya utekelezaji miradi ambapo wametekeleza miradi ya upandaji miti miradi 41, utengenezaji wa barabara miradi 6 na kilimo cha mbaogamboga miradi 25.
Baada ya ziara hiyo amesema vikundi vingi vimefaidika na miradi hiyo na kwamba walengwa wengi wameweza kujiongezea kipato watoa huduma za jamii kutoka mitaa 72 wamaweza kupata mafunzo ya usimamizi wa miradi kamati nazo zimejifunza suala zima la manunuzi kwa kuzingatia ngazi ya jamii huku akitaja changamoto katika utekelezaji wa PWP ni upatikanaji wa maeneo ya utekelezaji wa miradi hiyo ndiyo maana kumekuwa na miradi midogo kuliko ile mikubwa.
Kwa upande wao wananchi hao wameishukuru TASAF na Manispaa ya Ilala kwa kuwajali kuwapa miradi ambayo imewasaidia kupata pesa ya kujikimu na kusaidia watoto wao wanaosoma shule mbalimbali.
Akisoma taarifa ya kikundi hicho, Afisa Maendeleo wa kata ya Jangwani Mwatanga Chaulembo , amesema wanchi hao wameomba mradi huo uendelee kwa kuwa umewasidia na kuwafanya kujifunza mambo mengi katika kuendeleza shughuli za kiuchumi na kusema kuwa katika mradie huo jumla ya miti 115 na 75 iko katika hali nzuri ambayo imepandwa katika barabara za Mtambani Matumbi , Congo na Nyati.
Post a Comment