Ads

Baraza la Wataalamu wa Maabara lavishauri vyombo vya kutoa elimu ya maabara kwa wananchi


Image result for picha za ummy mwalimu
Hussein Ndubikile
Mwambawahabari
Baraza la Wataalamu wa Maabara nchini limevishauri vyombo vya habari kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya kupata huduma ya vipimo kwenye maabara ambazo hazijasajiliwa  ili kuwapunguzia gharama ziisizo za lazima pamoja na kupewa vipimo visivyo sahihi.

Hatua hiyo imekuja baada ya taarifa ya kuwepo maabara zinazotoa huduma kinyume na sheria hasahasa zinazomilikiwa na watu binafsi hali inayosababisha mkanganyiko kwa wananchi kupewa vipimo visivyo sahihi vya magonjwa yakiwemo ya Malaria na Kisukari.

Hayo yamesemwa leo  jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi wa Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa, Daktari Charles Masambu wakati wa Semina fupi iliyotolewa na baraza hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Amesema kutokana na kuwepo maabara zisizotambulika kisheria wananchi wamekuwa wakipatiwa vipimo batili vya magonjwa hali inayowaongezea gharama ya kulipia vipimo na kununua dawa pasipo gundulika kuwa na maradhi yoyote.

“ Muwasaidie wananchi kuelewa maabara  zisizojasiliwa tuwaelekeze  vigezo vinavyotakiwa maabara itambulike kisheria mkifanya hivyo mtawasaidia wananchi kupata vipimo sahihi na kuwapunguzia gharama,” amesema.

Amebainisha kuwa sheria inamtaka muajiri kuwa na vigezo vinavyotambulika na kuajiri mtu aliyesajiliwa na baraza na kwamba kwenda kinyume na hapo ni kukiuka sheria zinazoongoza utoaji huduma wa maabara.

Amefafanua kuwa hadi sasa kuna maabara nane zenye viwango vya kimataifa na  33 zenye hadhi ya kuanzia nyota moja hadi nne.

Kwa upande wake Msajili wa baraza hilo, Dickson Majige amesema tayari baraza limeshaanza mchakato kutoa vitambulisho maalum huku akisisitiza wale watakaoshindwa kufanya mitihani hawatambuliwa na baraza hilo.

No comments