TIMU YA VIJANA YAZIDI KUFANYA VIZURI KOMBE LA DUNIA URUSI, YASHINDA MECHI ZOTE ZA MAKUNDI.
Mwambawahabari
Tanzania imefanya vizuri Sana katika hatua ya makundi. Imeshinda mechi zote.
Haijafungwa hata goli moja. Ndio timu ya kwanza kufunga goli katika mashindano. Tumezifunga timu zote katika kundi ambazo ni Kazakhstan goli moja kwa bila.
Na mechi ya pili tukaisambaratisha Urusi goli tatu kwa bila . Kwa hakika watoto hawa wanapiga soka sana. Sisi timekua kivutio cha watu kwa kushangiliwa na kupiga soka kila mtu sasa anatuzungumzia.
Huyo ni Mbunge wa Urusi alikuja kwanza kutoa salamu kikosi cha Tanzania na kupiga picha. Anaitwa Michael Digtyorov.
Timu ya Tanzania ya watoto wa kike inayoshiriki mashindano ya kombe la dunia la watoto wa mitaani kwa programu ya Street Child World Cup :Future depends on you tayari tumeshafuzu hatua ya robo fainali.
Kikosi cha Tanzania kikiwa na mkutano mfupi asubuhi baada ya kupata chai ya asubuhi na huku Mkufunzi Rogasian Kaijage akitoa maelekezo na anapoongea Mama Sue ambae ni Mjerumani ambae ndio Mkuu wa Kundi zima ndugu Mohamed Mansour Nassor anakua anatafsiri.
Tanzania imefanya vizuri sana hatua ya makundi kwa kuzufunga timu za Kazakhstan goli moja kwa sifuri huku mechi ya pili wakiichambanga na wakiisambaratisha timu ya wenyeji Urusi goli tatu kwa sifuri.
Nahodha wa Tanzania Asteria Robert akihojiwa na waandishi wawakilishi wa BBC Africa na ndugu Mohamed Mansour Nassor akiwa anatafsiri lugha ya Kiswahili kwenda Kiingereza na Kiingereza kwenda Kiswahili.
Tumemaliza vinara wa kundi A na tutacheza robo fainali na Marekani baada ya Wamarekani kuwafunga Mafarao wa Misri goli 3-1.
Tanzania imekuwa ni kivutio kwa aina tofauti sana katika mashindano haya na tunajitahidi kwa kila njia kuhakikisha kuwa tunaibuka washindi na kuipaisha nchi yetu kimataifa.
Tanzania ndio bingwa wa kombe hili kwa mwaka 2014 huko nchini Brazil na mwaka 2010 ilicheza nusu fainali huko Afrika ya Kusini.
"Katika mechi za leo tumefanya vizuri kwani sisi Tanzania tumekua timu ya kwanza kupachika bao pekee wavuni kabla ya nchi zengine" .alisema
Pia sisi tuna clean sheet yani hatujafungwa hata goli moja lakini pia vijana wetu wana ujuzi wa Kucheza mpira wa aina yake katika techinical skills.
Pia timu inashangiliwa sana na kuzungumzwa na wanaulizia kuhusu Tanzania na waandishi wa habari wa vyombo vya Urusi na vya kimataifa kama BBC wanagombea Tanzania kuwafanyia wachezaji mahojiano nao na pia BBC Africa Tanzania itarushwa hewani katika habari za michezo.
"Katika Utalii tukitaja Mlima Kilimanjaro na Zanzibar ndio kabisa wanazidi kuelewa nchi yetu Vijana wanaimba Tanzania Tanzania na sisi wote huku wakimtaja Rais John Magufuli na kusema tumekuja kufanya kazi tu huku wakisema Hapa Kazi Tu" alisema.
Taarifa hii ni kwa hisani ya Tanzania Russian Alumni Association.
Post a Comment