Ads

DC MJEMA AZINDUA RASMI KAMPENI YA UJENZI WA CHOO CHA MTOTO WAKIKE SHULE ZA MSINGI WILAYA YA ILALA.

 Mwambawahabari 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amezindua kampeni ya  ujenzi wa  Vyoo vya mwanafunzi wa kike katika halmashauri hiyo ambapo amechangia kwa kujenga Matundu 40.

Mjema amesema hayo leo katika hafla iliyoandaliwa na watumishi wanawake wa halmashauri ambapo wameunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kukabiliana na changamoto zinazomkabili mototo wa kike na kuamua kuzindua kampeni hiyo ili kusaidia watoto wa kike wanoashindwa kufika shule siku 3 hadi 4 za kila mwezi.

Amesema katika halmashauri ya Ilala wanapaswa kujenga vyoo 3000 na kwa jambo hilo walilolianzisha kujenga vyoo hivyo kutapunguza changamoto ya vyoo na kuongeza kuwa kuna taasisi inayofahamika kama Shia koja ya kutoka Uingereza wameahidi kuchangia kujenga choo kimoja chenye matundu 6.

"Tunataka tuwasaidie wanafunzi wa kike kwa kujenga vyoo vyenye kila kitu ndani ili wasiwe wasumbuka na kuwaza kuingia gharama yoyote yakujisitiri" Amesema Mjema.

Aidha amewataka wanawake waendelee kuchapa kazi kwa bidii ili kuweza kukuza maendeleo ya manispaa hiyo pamoja na taifa kwa Ujumla.

Kwa upande wake Afisa Elimu msingi Elizabeth Thomasi amesema halfa hiyo inafanyika kila mwaka ambapo wanasheherekea kwa kupongezana lakini kwa mwaka huu imekuwa ya tofauti kwani wameamua kutatua changamoto za mtoto wa kike na kuanzisha kampeni hiyo.

Hafla hiyo iliyofanyika leo imehudhuriwa na wafanyakazi wa Idara mbalimbali za halimashauri  ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Pia katika hafla hiyo Watumishi hao wamemkabidhi Zawadi Dc Mjema kutokana na Kuchapa kazi kwa Mkuu huyo ambapo amejitoa kuwatumikia wana Ilala kwa nguvu zake zote na kwa Moyo.

No comments