Ads

Miji sita yakukumbwa na tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani

 Na. Hussein Ndubikile.
Mwambawahabari. 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imetoa Ripoti ya Taifa ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani nchini ambapo ripoti hiyo imeabini  jumla ya watoto 6,393 wanafanya kazi wakati wa mchana  huku  1,385 wakati wa usiku.

Ripoti hiyo imetokana na tafiti iliyofanywa na wizara hiyo pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa msaada wa kiufundi kutoka Shirika la Railway Children ambapo ilifanyika kwa muda mfupi kwenye miji sita ikiwemo Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Mwanza na Arusha.

Akizungumza wakati wa kuzindua  ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto , Sihaba Nkinga amesema ripoti inatoa matokeo ya utafiti wa watoto wenye umri kati ya miaka 0-18 ambao wanaishi na kufanya kazi katiika Miji sita na kwamba wakati wa mchana idadi ya wavulana ilifikia asilimia 76 ya watoto wote waliohesabiwa wakati wasichana ilifikia asilimia 24.

“ Wakati wa usiku idadi ya wavulana ilipungua  kwa asilimia 70  wakati huo  idadi ya wasichana  iliongezeka  kufikia asilimia 30,” amesema.
Amebainisha kuwa kuongezeka kwa idadi ya wasichana wakati wa usiku ilitokana na kuongezeka kwa wasichana wenye umri mkubwa  ktai ya mika 15- 18  wanaojishughulisha na biashara ya ngono.
Amefafanu kuwa ripoti imebaini watoto wenye umri mkubwa walikuwa hawajihusishi na sughuli ya kuombakuomba  bali walikuwa wakifanya biashara zinazohamishika huku akiongeza utafiti pia uligundua kwamba asilimia 50 ya watoto waaoishi na kufanya kazi mitaani ni wenye umri wa miaka zaidi ya miaka 15.

Amesisitiza kuwa ripoti hiyo imebaini vijana 4,202 wenye umri kati ya miaka 19-25 ambao wanaishi na kufanya kazi mitaani.

Amezitaja sababu zinazochangia watoto kuingia mitaani ni kuvunjika kwa ndoa, ukatili wa kijinsia pamoja kukosa mahitaji muhimu na kwamba lengo la Serikali kupunguza changamoto hiyo kwa asilimia 50 hadi kufikia watoto 3,000 au chini ya hapo.

Sihaba amesema katika kuhakikisha idadi ya watoto wanaoishi mitaani inapungua serikali inaendelea na juhudi za kuwafanya wananchi wake wafikie uchumi wa kati na kuboresha huduma ya elimu bure shuleni kuanzia Shule za Awali hadi kidato cha nne.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Kanda ya Afrika Mashariki, Pete Kent amesema utafiti huo umefanyika katika miji hiyo ambapo kwa kiasi kikubwa jiji la Dar es Salaam limebainika kuongoza kwa idadi kubwa ya watoto wanaoingia mitaani sababu kubwa ikitajwa kuvunjika kwa ndoa na ukatili.


Pia amesema shirika hilo litaendelea kufanya jitihada kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau ili kuhakikisha idadi ya watoto hao inapungua.

Aidha amesema hali hiyo ikiachwa iendelee itatishia ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla hivyo jitihada za dhati zinatakiwa kufanywa ikijukuisha jamii na mamlaka husika.

Katika hatua nyingine amesema watafiti walioshiriki waliangalia maeneo muhimu wakati wa utafiti huo yakiwemo ya kiini cha tatizo, sababu na jinsi ya kutatua changamoto hiyo.

No comments