(KWESE) TV 1 NA TBC ZA UNGANA KURUSHA LIVE MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA
Mwamba wa habari
Na.John Luhende
KFS Tanzania imesema itaanza rasmi kurusha matangazo ya moja kwa moja ya michuano ya mpira wa Kombe la Dunia ( FIFA ) word cup 2018 itakayofanyika fanyika nchini Urusi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa KFS Joseph Sayi amesema kuwa KFC itarusha matangazo hayo kwa kushirikiana na Kituo cha Televisheni ya Taifa TBC na kwamba matangazo hayo yatarushwa moja kwa moja kutoka nchini Urusi.
"Michezo ni moja ya burudani zinazo pendwa Sana Tanzania na Duniani hivyo KFS Tumeamua kuwapa burudani watazamaji wetu watazame KFS/ zamani TV1 na TBC kushuhudia mech zote" Amesema.
Aidha amesema Mkurugenzi wa Masoko TBC wamefurahishwa kufikia kwa hatua hiyo ya ushirikiano heshima kubwa kwao kama Shirika la Utangazaji nchini na kwamba wanatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na KFS Tanzania kwa kuwaunganisha Mamiloni ya watanzania watakao tazama michuano hiyo bila malipo yoyote.
Ikiwa
ni channel pekee ya bure ya michezo nchini KFS Tanzania imejitengenezea
wasifu kwa kuzalisha vipindi bora zaidi hapanchini na barani Afrika hadi vya
kimataifa vinavyosimamiwa endana na watazamaji wake.
"Ni jambo la furaha kwetu
kuleta Kombe la Dunia 2018 kwa Watanzania pia ni nyenzo ya kukuza na kuimarisha
Uhusiano wetu na watazamaji hususani mashabiki wa michezo ya kila aina
wanaotusogeza na lengo letu ikiwa ni kuwasilisha burudani kupitia nyenzo
mbalimbali ikiwemo kurasini zetu za kijamii kama sehemu ya kusambaza
ujumbe wetu wa burudani bure "Amesema Gillian Rugumamu.
Pamoja
na michuano amesema timu ya uzalishaji vipindi ya KFS imeandaa Studio ya aina
yake kuelekea kurusha matangazo zitakapo Rukanuga preview, highlight na mechi
moja kwa moja zitakazo fanyiwa uchambuzi na wadau pamoja na watangazaji kwa
lugha ya kiswahili, ambapo kwa mujibu wa Msimamizi mkuu wa eneo hilo
Mukhsin Mambo Studio itakuwa na Usha wishing wa wakereketetwa.
Kutakuwa
na mechi 32 zikiwemo zitakazo chezwa na timu za Afrika Robo fainali, Nusu
fainali pamoja na mechi ya mwisho ya fainali ambapo ufunguzi utafanyika tarehe
14 June 2018, KFS Itapatikana kupitia channel 103 startimes , Continental
channel 07 pamoja na Ting channel namba 36.
Post a Comment