Ads

HAKUNA MTU ALIYETHIBITIKA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA NA HAKUNA UGONJWA HUU TANZANIA. NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari, viongozi wa Wizara na wawakilishi wa WHO wakati
akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa Ebola mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es
salaam.





Waandishi wa Habari kutoika vyombo mbali mbali wakifuatilia kwa makini tamko kuhusu gonjwa wa
Ebola alilotoa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine

Ndugulile akisisitiza mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

Mwamba wa habari
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto dkt. Faustine
Ndugulile amethibitisha kuwa hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa EBOLA
hapa nchini wala hakuna ugonjwa huo hapa Tanzania.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari wakati
akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa EBOLA kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya
habari kuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini.

“Napenda kuwatoa hofu watanzania kwamba hakuna ugonjwa wa EBOLA na wala
hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo, hivyo tuendelee na shughuli za
kujenga Taifa ila tunatakiwa tuchukue tahadhari za kujikinga juu ya ugonjwa huu”
alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa
EBOLA usiingie nchini Serikali imeweka vifaa vya kupima joto la mwili (themo
scaner) pia wapo wataalamu wa Afya ambao wanauliza hali ya wageni wanaoingia
katika mipaka yote inayoizunguka nchi yetu ili kuzuia ugonjwa huo kuingia.

Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa, Serikali haijafunga mipaka ya nchi kwa sababu ya
kujikinga na EBOLA.

"Tanzania hatujafunga mipaka na hatuwezi kufunga biashara za mipakani ila
tumeimarisha ufuatiliaji wa watu wanaoingia nchini hususani maeneo ya viwanja vya
ndege na mipaka mingine yote."

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameitaka mikoa yote iliyo mipakani kudhibiti watu wote
wanaoingia nchini kwa njia za panya ili kuepusha uingizaji wa ugonjwa huo kwa
wananchi huku akiwataka wafanyabiashara wa mipakani kutoa ushirikiano ili
kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani ambaye pia ni Afisa wa
kushughulikia magonjwa ya kuambukiza Dkt. Grace Saguti amesema kuwa Wananchi
wanatakiwa kupata elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

“Elimu inahitajika ya kutosha kwa wananchi wote hasa katika kufichua wagonjwa wa
Ebola kama watagundulika hasa wanaotoka nje ya nchi ili kupata msaada kutoka
kwa watoa huduma za afya walio yao juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

No comments