Ads

DC MJEMA AWATAKA WANUFAIKA WAMPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI ILALA , KUHITIMU.

Mwamba wa habari
Na John Luhende
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi wanaonufaika na mfuko wa kunusuru kaya masikini TASAF Manispaa ya Ilala kutumia vema pesa Wanazopata katika mpango huo na kuweka malengo ya kiuchumi.

Mheshimiwa Mjema Ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika katika kutembelea miradi ya maendeleo wilayani humo inavyotekelezwa na TASAF katika kata mbalimbali Wilayani  Ilala.


"Ni singe penda kuona ninyi mnategemea TASAF  kila mwaka  ifike wakati (mgruate) mhitimu ili wasaidiwe na wengine, miradi yote inayobakishwa na TASAF muiendeleze isije ikiisha hewani."Alisema
Amewahimiza Wananchi hao kutojiweka  katika hali ya unyonge bali wa bali wachangamkie miradi na kuifanya kwa moyo ili iwaletee  mafanikio.

Aidha amewataka maafisa Ugani kuwasaidia wanachi wanaofanya kazi ya kulima bustani za mbogamboga kulima kitaalamu kuliko ilivyo hivi sasa ambapo wanalima kienyeji na kujikuta wakipata faida kidogo.
"Hongereni kwa kuwa mmefanyakazi lakini lakini huu si utaratibu mzuri wa kulima bustani na hii ni kazi ya maafisa Ugani naomba hawa wananchi wasiachwe hivihivi wasaidiwe walimu kisasa. Amesema
Kwa upandwe wao wanufaika wa miradi ya kunusuru kaya Masikini TASAF  katika  maeneo yaliyotembelewa ya  Tabata Liwiti, Segerea, na Kitunda kati wameishukuru serikali na manispaa ya Ilala kwa kuwapa miradi yake  kwani imewasidia katika kuendeleza maisha yao.

‘’Mimi nilikuwa nimejenga nyumba yangu haina bati ,  lakini kwa mradi huu wa TASAF jinni nilikuwa napata hiyo hela  nimejiwekeza nikanunua magunia ya mkaa nikawa nauza  na nikanunua mabati nikaezeka nyumba yangu vyumba viwili  ,choochangu kika bomoka nashukuru mungu nikajiwekeza tena kwa hizi hela za TASAF  nikachimba  na nikajenga  choo change hadi sasa najihifadhi.Alisema  Mwana asia Biligenda mazi wa Liwiti.


‘’TASAF naishukuru sana mpaka hapa nilipofikia mimi nimejifunza  ushonaji kutokana na hele ya TASAF  nikaanza ushonaji na sasa nimenunua  Mashine nashona mashuka nauza na kukopesha na wateja ninao sasa natafuta flemu ilinifungue ofisi yangu ya ushonaji  nashukuru sana serikali .Alisema  Zainabu Ausi.
















1 comment:

  1. Big up TASAF na Malkia wa nguvu na Mchapakazi makini Mh.Mkuu wa Wilaya

    ReplyDelete