Ads

DC MJEMA AFUNGUA MAONESHO YA WAJASILIAMALI ILALA


Mwambawahabari
Mkuu  wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema  amesema Wajasiliamali wa Wilaya hiyo watashiriki katika maonesho ya ujasiriamali kwa ajili ya kutangaza biashara zao.

DC Mjema amesema  maonesho hayo ya bure  siku nne yanatarajia kuzinduliwakesho Ijumaa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

"Halmashauri ya Manisipaa ya Ilala imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika kuwaibua, kuwawezesha, kuwaelimisha na kuwaendeleza  wajasiriamali wadogo wa kati na wakubwa kupitia mpango bajeti kwa kuzingatia Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM"amesema

Mjema amesema  manispaa ya Ilala imetenga siku nne za maonyesho ya biashara wajasiriamali mbalimbali waliopo Ilala watatangaza bidhaa zao.

Alisema pia watatoa tuzo kwa mabanda bora ya biashara ambayo yameonyesha ushindani katika maonyesho hayo kwa mwaka huu 2018.

Aidha alisema Ilala ina takriban wajasiriamali 15,000  ambao wapo katika vikundi vikubwa na vidogo wenye shughuli za pamoja na mmoja mmoja    .

Mjema alisema katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2014 ,2015,2017 hadi 2018 Ilala imekuwa ikitenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ili kuwawezesha wajasiriamali hao katika mfuko wa kujiendeleza wanawake na vijana.


"Katika mpango huu wa kusaidia vijana jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimekopeshwa kwa vikundi vya wanawake na vijana 2,978  ambapo kati yao vijana 8,482 na wanawake 6,906  walinufaika "Amesema .

Akielezea changamoto katika jitihada mbalimbali  za kusaidia vikundi alisema wajasiriamali wengi hasa wadogo hushindwa kunufaika na mfumo huo kutokana na masharti mbalimbali.

Mjema alisema kutokana na changamoto hizo wamezingatia maelekezo serikali ya awamu ya tano kupitia viongozi mbalimbali na kufanya maboresho ya mfumo huo ili kukidhi mahitaji ya wajasiriamali.

No comments