BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO LAPITISHA BAJETI YA MATUMAINI,LAWEKA VIPAUMBELE VITAKAVYOTATUA KERO ZA WANANCHI
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ndani ya ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Kibamba limepitisha bajeti ya matumizi sambamba na vipaumbele vyenye tija kwa ajili ya kutatua kero za wananchi, kwa mwaka 2018/2019 Halmashauri imekadiria kutumia fedha kiasi cha Tsh.
98,238,193,600.00. Kati ya fedha hizo Tsh. 76,607,163,700.00 ni matumizi ya kawaida na mishahara ambayo ni sawa 78%
Tsh. 21,631,029,900.00 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 22 ya bajeti yote Kwa mwaka 2018/2019 Halmashauri itatumia jumla ya Tshs. 71,796,915,600.00 ikiwa ni ruzuku, sawa na 100% kutekeleza vipaumbele vya maendeleo na maeneo ya utoaji wa huduma.
Kati ya fedha hizi mishahara ni Tsh. 61,923,432,600.00 ikiwa ni mishahara, matumizi ya kawaida ni Tsh.1,593,213,500.00 na miradi ya maendeleo ni Tsh. 8,280,269,500.00.
Aidha Manispaa ya Ubungo kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 itatumia Tshs. 25,691,278,000.00 kutoka katika mapato ya ndani kwa matumizi mengineyo, mishahara, miradi ya maendeleo na uchangiaji (Cost sharing).Tshs. 12,600,760,400.00 zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo sawa na asilimia 49% na Tshs. 8,307,173,600.00 sawa na asilimia 32% zitatumika katika maeneo ya uendeshaji wa shughuli za ofisi na Tshs.191,544,000.00 sawa na asilimia 1% zitatumika katika kulipa mishahara ya watumishi na Tsh. 4,591,800,000.00 ni uchangiaji (cost sharing).
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imekidhi kigezo cha kutenga asilimia 60 ya fedha za mapato yake ya ndani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Jumla ya Tsh. 12,600,760,400.00 sawa na asilimia 60 ya fedha za mapato ya ndani imetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Tsh.8,498,717,600 sawa na asilimia 40 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara
Katika kufanikisha malengo hayo bajeti ya mwaka 2018/2019 imeweka vipaumbele katika maeneo mbalimbali,baadhi ya vipaumbele hivyo ni kama ifuatavyo:
kuimarisha utawala bora na utoaji huduma kwa jamii kwa kujenga jengo la ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ambapo kiasi cha Tsh 3,000,000,000/- kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Jengo hilo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kuongeza na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielektroniki kutoka Tsh. 22.5 Bilioni kwa sasa hadi Tsh. 25.7 Bilioni kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Kuboresha utoaji huduma kwa wananchi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo hivyo Kiasi cha Tsh. 21,631,029,900/= kimetengwa kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kununua madawa na vifaa tiba, Kujenga na kuboresha miundo mbinu ya afya katika hospitali ya Sinza, Vituo vya Afya na zahanati. Jumla ya Tsh. 8.2 Bilioni zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kuboresha miundombinu ya barabara kwa kujenga Madaraja/Makalvati, barabara kwa kiwango cha lami, kufanya matengenezo ya kawaida ya barabara, muda maalum, maeneo korofi, njia za waenda kwa miguu, Ujenzi wa vivuko vya waenda kwa miguu na Mifereji katika barabara za Manispaa. Jumla ya Tsh. 1.4 Bilioni zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kukuza uchumi na kujenga miundombinu katika sekta za afya, elimu, maji na masoko kwa kutwaa ardhi, kulipa fidia maeneo yaliyotwaliwa kwa ajili ya uwekezaji hivyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Kitengo cha Uthamini kimetengewa Tsh.1,200,000,000/= kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.
Kutoa mikopo kwa wanawake na vijana kwa mujibu wa miongozo ya Kitaifa ili kuchochea maendeleo na ukuaji wa kipato kwa wananchi ambapo kiasi cha Tsh 1,144,428,098/= kimetengwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kujenga na kuboresha majengo ya utawala na miundombinu, ofisi za walimu Shule za Msingi na Sekondari kiasi cha Tsh. 300,000,000/= kimetengwa katika mwaka wa fedha 2018/2019.
Kuboresha huduma ya usambazaji maji safi na salama kwa wananchi hivyo Kiasi cha Tsh.1,303,129,500/= kimetengwa kwa ajili ya Miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Kupanua wigo wa kutolea huduma za afya kwa jamii kwa kujenga Hospitali ya Wilaya ya Ubungo.Hivyo kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa mil.100,000,000 kwa ajili ya hatua za awali.
Kuendelea kuboresha na kujenga masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Kiasi cha Tsh. 450,000,000/= kimetengwa katika bajeti ya mwaka 2018/201 nakadhalika.
IMEANDALIWA NA :
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
MANISPAA YA UBUNGO.
Post a Comment