Ads

UWT KINONDONI USHINDI BILA RUSHWA KINONDONI INAPENDEZA



Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
WANACHAMA wa Umoja wa Wanawake UWT wametakiwa kujiami na kupita kuomba kura kwa mgombea wao wa ccm jimbo la KINONDONI Maulidi Mtulia bila kutoa rushwa.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam Jana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa Amina Makilagi wakati wa mkutano wa tathimini ulioandaliwa na UWT jimbo la Kinondoni .

" Wanawake wenzangu uchaguzi  huu ccm tunashinda kwa kishindo kwa mgombea wetu Mauld Mtulia   msitumie rushwa  naomba UWT muwe Kifua Mbele tusubiri siku  ifike apishwe aweze kusaidia wana Kinondoni na wanawake kwa ujumla" alisema

Makilagi aliwataka wanawake wa UWT kulinda shahada zao za kupiga kura siku ifike ya February 17 wajitokeze kwa wingi katika vituo kupiga kura.
.
Alisema jimbo hilo la ccm na litabaki kuendelea kuwa mikononi mwa ccm.


Aidha  alisema MAENDELEO yanaletwa na  ccm kwa kutekeleza ilani hivyo wasirubuniwe kupigia upinzani  .


" Wanawake wenzangu wa jimbo hili wengi wajasiriamali hivyo Mara baada kuapishwa wasimamie waweze kupata mikopo ya wanawake na vijana" alisema

Aliwataka wana Kinondoni wamchague Mtulia kwani ni mnyenyekevu pia mwadilifu   MTU mwenye maadili mazuri mwana zuoni .

Kwa upande wake Mgombea ubunge huyo  Maulid Mtulia aliwapongeza wanawake wote wanaomuunga mkono pamoja na wana Kinondoni.

Mtulia aliwakikishia wananchi wa jimbo hilo kuwa yeye ni mchapa kazi  sio mbabaishaji .

" Nichagueni changamoto zote nitasimamia ndani ya jimbo langu
Wanawake na wana Kinondoni tutashirikiana kukuza MAENDELEO."alisema Mtulia.

No comments