UWT Ilala yawataka wanachama wake kuvunja makundi na kuacha nongwa.
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
UMOJA wa Wanawake ( UWT) Ilala yawataka wanachama wa chama hicho kuvunja makundi na kuacha nongwa wote wasimamie misingi ya chama .
Hayo yalisemwa Dar es salaam Jana,na Mjumbe na Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya ya Ilala Batuli Mziya katika uzinduzi wa miaka 41 ya Chama cha Mapinduzi CCM UWT kata ya KITUNDA.
Batuli alisema katika chama makundi sio mazuri yanarudisha nyuma uhai wa chama na kurudisha nyuma MAENDELEO ya chama cha mapinduzi na jumuiya zake.
" Tupo katika wiki ya kuzaliwa ccm kutimiza miaka 41 chama hichi kilizaliwa February 5 mwaka 1977 tunashiriki katika kazi za chama na kukienzi " alisema Batuli.
Alisema lengo la UWT kutekeleza Ilani na kusimamia misingi ya chama
Kiweze kufikia malengo na kuakikisha kinashika dola na wanawake ndio jeshi la chama .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Amina Dodi alisema yeye kama Mwenyekiti wa jumuiya hiyo leo ameelekeza msafara wake katika zahanati ya KITUNDA kushiriki usafi ,kufanya kazi za kijamii na kugawa maziwa kwa wagonjwa waliofika katika zahanati hiyo leo
Dodi alisema ndani ya wiki hii jumuiya yake itandua kazi za chama ngazi ya kata na jimbo na kila jimbo itafanya mpaka kufikia tarehe tano mwezi huu.
Alisema amewapangia majukumu mbalimbali ikiwemo uchangiaji wa damu .
" UWT Ilala INA wanachama 25000 matawi 210 wanachama wote hai na mikakati ya jumuiya yake wanatarajia kuanza ziara hivi karibuni kujenga chama.
Naye Mwenyekiti wa UWT KITUNDA Doreen Malo .amempongeza magufuli kwa kazi nzuri amewataka wanawake kumsaidia Rais.
Mganga Mkuu wa zahanati ya kata Peter Kavishe,Zahanati hiyo ilianza kutoa huduma kuanzia mwaka 1977 kwa siku inapokea wagonjwa 150.
Kavishe aliwapongeza UWT KITUNDA kwa msaada huo walioonyesha katika zahanati yao kongwe.
Mwisho
Post a Comment