Ads

UCHUMI CUP YAFUNGULIWA HANDENI KUHAMASISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA VIJANA

Katika kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za maendeleo hususani kilimo mashindano ya mpira wa mguu na mpira wa pete UCHUMI CUP yamefunguliwa rasmi kwa ngazi ya robo fainali na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mapema mwishoni mwa wiki.




Akifungua mashindano hayo kwenye viwanja vya Kigoda Stadium Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi.Upendo Magashi alisema kuwa michezo ni furaha na amani hivyo fursa hiyo itumike kukuza vipaji lakini pia kujiunga katika vikundi vya uzalishaji hususani kilimo ukizingatia Handeni shughuli kuu ni kilimo.




Aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuhakikisha vijana wanatumia vipaji walivyonavyo katika kuhakikisha wanainua uchumi wao na kuendana na falsafa ya Mh. Rais ya HAPA KAZI TU!.




Kwa upande wake mratibu wa mashindano Bw. Baraka Nkatura alisema kuwa Mashindano yalianzishwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe na kuamua kuyatumia kwenye msimu huu wa kilimo ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiinua kiuchumi.




“Tunaamini mbali ya kukuza mahusiano baina yetu, tutaweza kubadilishana uzoefu utakaotusaidia kukuza vipaji vyetu na kujiinua kiuchumi” alisema Mratibu.


 Kaimu
Katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi akifuatiwa na waratibu WA
michezo wakisalimiana  na Timu na uongozi wao kabla ya mechi kuanza

No comments