RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA OFISI ZA BAKWATA, MUFTI ATOA NENO ZITO KWA WAISLAMU WATAKAO KWENDA KINYUME.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipeana mkono na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaji Mussa Salum leo wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa ofisi za BAKWATA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza wakati wa ukaguzi wa ofisi za BAKWATA leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu pamoja na waandishi wa habari wakifatilia mazungumzo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja Mufti
Mkuu wa Tanzania
Sheikh Abubakary Zubeiry.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry akizungumza na waandishi wa habari.
Ujenzi wa Msikti mkubwa ukiwa unaendelea kujegwa katika Wilaya ya Kinondoni karibu na ofisi za BAKWATA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua ujenzi wa Ofisi za BAKWATA
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry akiomba dua baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumaliza ukaguzi wa ujenzi wa ofisi na msikti. (Picha zote na Noel Rukanuga)
.....
MWAMBA
WA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Viongozi
wa dini nchini wametakiwa kuwa mstali wa mbele katika kufanikisha masula ya
kimaendeleo ikiwemo ulipaji wa kodi pamoja na
kuliombea taifa ili liendelee kuwa na amani na uwajibikaji kwa watanzania
wote.
Akizungumza
leo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Ofisi za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amesema kuwa viongozi wa dini bado
wana kazi kubwa ya kuhakikisha watanzania wanakuwa na amani na kuchangia katika
ujenzi wa taifa.
Amesema
kutokana umuhimu wa viongozi wa dini, serikali itaendeleo kuwapa ushirikiano
ili kuhakikisha wanafanya kazi ya mungu katika mazingira rafiki.
“Nafasi
ya Mufti ni kubwa sana hivyo tumeona ni vema kupatikana kwa ofisi kubwa ambayo itampa
fursa ya kukaa faragha na mungu jambo ambalo ni jema katika kuhakikisha anatoa
huduma kwa waumini ya dini ya kislamu katika mazingira bora” amesema Mhe Makonda.
Amesema
kuwa mazingira ya ofisi ya awali yalikuwa sio rafiki kutokokana na kelele
zilizokuwepo eneo hilo ambazo zilikuwa ni changamoto wakati Mufti Mkuu wa
Tanzania akifanya kazi yake.
Makonda
ameeleza kuwa makoa makuu ya BAKWATA yanapaswa kuwa na mazingira bora ili viongozi
wa dini wanapokuja kutoka nchini mbalimbali waweze kufika sehemu mzuri.
“Pia
kuna msikiti mkubwa unajengwa hapa nchini ambao unauwezo wa kuchukua waumni
zaidi ya 6,000 ambapo utakuwa mkubwa kuliko yote afrika mashariki ”amesema
Makonda.
Hata
hivyo amefafanua kuwa baada ya kukamilika kwa ofisi hizo wataangalia namna ya
kupiga hatua zaidi katika kuahakikisha BAKWATA inakuwa na maendeleo.
“Naomba
BAKWATA mnipe orodha yote ya viwanja ambavyo umedhulumiwa ili muweze kuvipata
na kufanya maendeleo” amesema Makonda.
Kwa upande wake Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakary Zubeiry bin Ally amemshuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye
amekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha ujenzi wa ofisi za BAKWATA.
Amesema kwa muda wa miaka 50 mpaka
sasa BAKWATA haijawai kuwa na ofisi kubwa ambayo ni rafiki katika kuhakikisha
wanafanya kazi zao.
“Tulikuwa tanapata changamoto
kubwa pale tunapoona viongozi wa dini kutoka nje ya nchi kuja kututembelaea
kutokana na ofisi zetu kuwa na mazingira sio rafiki kwani kuna kelele zinazotokana na sauti za watu wanaoishi na kufanya biashara karibu na ofisi zetu " amsema Mufti Zubeiry.
Amesema kutokana hali ujenzi huo
ambao unaendelea vizuri ni jambo jema kwa BAKWATA, huku akiwataka waumini wa dini ya
kislamu waendelee kufanya kazi ya mungu kwa umakini na kujiepusha na mambo
ambayo sio rafiki.
“Kiongozi wa dini ya ambaye
atakwenda kinyume na BAKWATA tutamtumbua ili sisi tuendelee mbele na sio
kuturudisha nyuma” amesema Mufti Zubeiry.
Hat hivyo Mufti Zubeiry ameeleza
kuwa wanaendelea kumuomba mungu ili mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na serikali
kwa ujumla waendelee na mpango wa kufanikisha maendeleo ya nchi.
“Waislamu tutaendelea kuliombea taifa na kukumbushana uwajibikaji kwa waumini wetu ili tuzidi kusonga mbele na
kufanikisha maendeleo ya taifa kwa ujumla” amesema Mufti Zubeiry.
Post a Comment