HALMASHAURI ZA MKOA WA TABORA ZIMETAKIWA KUOTESHA MITI MAJI MINGI KWA AJILI YA WANANCHI.
NA TIGANYA VINCENT- RS-TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewataka Wakurugenzi Watendaji wote mkoani hapa kuhakikisha wanaotesha miti maji kwa wingi katika vitalu vyao kwa ajili ya kuwauzia wananchi ili wapande katika maeneo hiyo.
Kauli hiyo jana na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Nathalis Linuma wakati zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega baada ya kupata taarifa ya kuwepo kuwa wapo baadhi ya wananchi wamekuwa waking’oa miti maji iliyopandwa mitaani kwa lengo la kupeleka kupanda katika maeneo yao.
Alisema kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi kung’oa miti hiyo na kuipeleka katika maeno yao vinaonyesha kuwa jamii imeanza kulikubali zoezi la upandaji miti kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira.
Linuma alisema kuwa ili kukabilina na uhitaji wa miti hiyo ni vema kila Halmashauri ikaoongeza idadi ya miche ya miti maji na matunda inayootesha kwa ajili kugawa au kuuza kwa wananchi.
Alisema kitendo hicho sio kitasaidia idadi ya miti inayopandwa bali hata kuongezea Halmashauri mapato kutokana uuzaji wa miti.
Awali akitoa taarifa ya zoezi la upandaji wa Miti katika Halmashauri ya Wilaya Nzega Jacob Ntalitinya alisema kuwa wanakabiliwa na wizi wa miti maji ambayo wameshaipanda katika baadhi ya maeneo ambayo hana ulinzi au nyumba jira kwa wananchi kuing’oa kwa ajili ya kuipanda makwao.
Alisema kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo wameamua kupanda aina nyingine ya miti ambayo wananchi haipendi.
Mpango wa Mkoa wa Tabora ni kupanda miti maji na matunda katika maeno miji na katika Taasisi za umma kwa ajili ya kuyapndesha maeneo hayo
Post a Comment