Ads

UMMY MWALIMU : UTEKELEZAJI MALIPO KWA UFANISI UMELETA TIJA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema utekelezaji wa mpango wa malipo kwa ufanisi (RBF) Wilayani Rufiji umeleta mabadiliko makubwa katika Vituo vya afya na Zahanati kwa uboreshaji wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu.

Waziri Ummy Mwalimu akipokea mabango kutoka kwa wananchi yenye jumbe mbalimbali kuhusiana na changamoto za Afya, alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini.

Amesema hayo leo alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia RBF unaotekelezwa katika mikoa nane nchini.

Ameeleza kuwa  mabadiliko hayo katika sekta ya afya yamefanyika katika maeneo ya utoaji huduma, Uongozi na Utawala, Rasilimali watu, Mifumo ya usimamizi wa utoaji taarifa za afya, madawa na teknolojia ya afy.

"Mfumo huu umesaidia maboresho, uwajibikaji,ufanisi na usawa kwani dhana hiyo inamfanya mtoa huduma kulipwa kulingana na matokeo ya kazi yake ambayo amehakikiwa na hivyo kufanya vituo hivi kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na kuboresha miundombinu ya vitu," amesema.

"Tumeanza mpango huu katika mikoa 8,tumefanya tathimini kwenye vituo vya afya na zahanati zote za Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilaya ya Rufiji, tukabaini vituo vya afya na zahanati hazikuwa na viwango vya ubora unaotakiwa, tukaona tuwapatie  shilingi milioni 10 kila kituo vilivyokidhi kwa ajili ya kuboresha miundombinu" ameongeza.

Pia ameipongeza kamati ya afya ya kijiji cha Nyamwage kwa kutumia ipasavyo sh. milioni 10 kwa kuongeza urefu wa paa na kupaua, kuweka malumaru na kuongeza matundu ya choo pamoja na tundu moja la choo kwa ajili ya walemavu

No comments