ANAYE DHANIWA KUZAA NA MCHUNGAJI MWINGIRA,AFUNGUKA MAZITO MAHAKAMANI.
Akiongozwa na wakili Peter Swai kutoa ushahidi katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe ambaye ni raia wa Marekani, Dk William Morris, Dk Nyimbi aliiomba mwanaume huyo asilipwe kiasi cha fedha cha Sh 7.5 bilioni anazodai Kwa sababu yeye hakuwa na mahusiano na Mchungaji Mwingira.
Dk Nyimbi kupitia Wakili wake Swai aliomba Dk Morris asilipwe kiasi hicho cha fedha Kwa sababu yeye hajawahi kuwa na mahusiano na Mchungaji Mwingira na kwamba hicho anachokidai siyo madai halali.
Wakili Swai alimuuliza Dk Nyimbi anasemaje kuhusu madai ya mumewe Dk Morris, kuwa wewe na yeye mkapimwe HIV.
Dk Nyimbi alidai kuwa yeye mwenyewe huwa anautaratibu wa kupima na kwamba Kwa bahati nzuri sheria za Tanzania zinaruhusu.
Swai alimueleza Dk Phillips kuwa mumewe Dk Morris anataka mtoto wake akapime vinasaba (DNA).
Dk Phillips alidai kuwa mtoto huyo ni wa kwake yeye, Dk Phillis na hajasema ni wa Dk Morris wala wa Mchungaji Mwingira.
Pia ameiomba Mahakama iamiru gharama za kesi zilipwe na Dk Morris.
Dk Nyimbi alisisitiza Kukana kuzaa na Mchungaji Mwingira na kwamba Mchungaji huyo wala hajawahi kuujua mwili wake.
Dk Nyimbi alitoa utetezi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhini.
Alidai kuwa alifunga ndoa na Dk Morris mwaka 2001 katika Kanisa la Mtakatifu Albano.
Alieleza kuwa baada ya ndoa walikaa mapumziko kwa siku tatu katika Hoteli ya Starlight kisha wakahamia Muhimbili ambako alikuwa anaishi katika chumba kimoja akiwa katika mafunzo ya vitendo.
Alidai kuwa baada ya miezi mitatu Dr Morris alikwenda Marekani na kwamba Mawasiliano kati yao yalikuwa ya shida shida.
Alidai kuwa kutokana na hali hiyo alichanganyikiwa kwa kuwa madaktari wenzake walikuwa wakimuuliza anaondoka lini na kwamba alikuwa akilia tu.
Alidai kuwa alijaribu kwenda katika Ubalozi wa Marekani mara mbili kutafuta Visa ya kusafiria lakini ilishindikana hivyo akaamua kuendelea kusoma ili asije akakosa vyote.
Alidai kuwa Dk Morris baada ya miaka minane alikuja Tanzania Aprili 25, 2009 baada ya kupata taarifa anakuja alikwenda kumpokea katika uwanja wa ndege wa KIA.
Alidai kuwa baada ya kumpokea walilala katika hoteli iliyopo Moshi ambapo usiku huo alimuelezea historia ya maisha yake, kwa muda mrefu, aliomuacha.
Alimueleza kuwa anamsisha yake amezaa na ana mtoto wa mwaka mmoja. Alimueleza kuwa alimuoa akiwa na miaka 30 hivyo amezaa akiwa na miaka 38.
Alidai kuwa alimueleza alimsukuma kitandani. Alieleza Dk Nyimbi.
DK Nyimbi alidai waliporudi nyumbani kwao Kibaha mkoani Pwani alimwambia kwamba mtoto huyo wa kiume kazaa na mfanyabiashara ambaye yuko nje ya nchi anaitwa Baraka.
Alidai Dk Morris alisema ana kuna ili mtoto huyo aliyekuwa akiitwa David atakuwa wake kwa sababu anampenda mkewe lakini siku zilivyokuwa zikienda mumewe alimwambia kwamba mtoto huyo kazaa na Nabii Mwingira.
"Aliniambia naitwa Polisi Kibaha nikatoe maelezo kuhusiana na mtoto, nilikataa, nikapigiwa simu na Polisi Kibaha ndipo nilipoamua kwenda, niliambiwa kwamba mumewe wangu kalalamika kuwa nimebakwa na Nabii Mwingira na nimezaa naye mtoto." Alieleza Dk Nyimbi.
Alidai kuwa alipoulizwa na Polisi alikataa kwamba hakuna jambo kama hilo na kwamba hajawahi kubakwa wala kuzaa na Mchungaji Mwingira.
Katika kesi hiyo, Dk Morris ambaye ni raia wa Marekani pamoja na mambo mengine anaiomba mahakama hiyo imuamuru Mwingira kulipa Sh 7.5 bilioni kama fidia ya kuzini na kuwa na mahusiano na mke wake huyo.
Dk Phillips Nyimbi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Mchungaji Joseph Mwingira.
Pia anaomba itoe amari ya kwenda kupima Ukimwi kwa yeye, Mchungaji Mwingira na mkewe Phillis na ifanyike kipimo cha DNA kati ya mtoto na walalamikiwa hao.
Inadaiwa kuwa Mwingira na Phillis waliingia katika mahusiano muda usiojulikana bila ya kujali kuwa Phills alikuwa ni mke wa Morris na kwamba mara baada ya Morris kufanya uchunguzi juu ya mahusiano hayo mke wake alidai kwamba yeye alibakwa na Mchungaji Mwingira.
Iliendelea kudaiwa kuwa kubakwa huko kulipelekea siyo tu mke wake kuwa na ujauzito pia kulisababisha kuwa na matatizo ya afya.
Desemba 28,2011 Morris na Phills walifunga ndoa ya Kanisani na wakati wa mahusiano yao, Phillis na Mchungaji Mwingira wanadaiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na kubahatika kupata mtoto wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 9.
Mlalamikaji huyo anadai kuwa alitoa taarifa katika kituo cha polisi Kibamba ambapo walimueleza kuwa suala hilo ni la uzinzi ama udhalilishaji na haliwezi kuwa la kijinai na kushauriwa kufungua kesi ya madai.
Kitendo cha mke wake kuwa na mahusiano na Mwingira ni kwenda kinyume na ndoa yao halali na kwamba kitendo hicho kimeharibu mipango yake ya mbele kiasi cha kumfanya apoteze hata matumaini ya kuendelea kuishi.
Pia kimemuaibisha na kushusha hadi yake siyo tu Tanzania na Duniani hivyo kumsababisha ateseke kiakili na kiuchumi.

Post a Comment