PICHA ZA ZARI , THE BOSS LADY AKIWASILI DAR , KUZINDUA DUKA KUBWA LA DANUBE.CAMERA YA MWAMBA YA WEKA MAMBO MUBASHARA..
Mwambawahabari
Balozi wa kampuni ya GSM ,Zarina Hasan , (boss Lady) akiwasili
katika uwanja wa nde wa kiamataifa wa Mwalimu JK Nyerere akitokea Africa ya
Kusini (Picha zote na Johnh Luhende, mwambawahabari)
Balozi wa kampuni ya GSM ,Zarina Hasan , (boss Lady) akiwasili katika uwanja wa nde wa kiamataifa wa Mwalimu JK Nyerere akitokea Africa ya Kusini (Picha zote na Johnh Luhende, mwambawahabari)
Zarina Hassan, akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege akitokea Afrika kusini ili kushiriki katika uzinduzi wa duka jipya la Danube lilopo mlimani city hapo kesho
Zari akiwa pamoja na mlinzi wa Diamondi ,wakielekea katika gari lao tayari kwa kuanza safari kueleke mjini.
Gari aliyopanda Zari pamoja na wenyeji wake waliofika uwanja wa ndege kwa ajili ya kumlaki kwa ajili ya shuhuli ya uzinduzi wa duka jipya la Danube mlimani City, hapo kesho
BALOZI wa Kampuni ya GSM, Zarina Hassan(Zari) amewasili leo Airport jijini Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini kwa lengo la kuzindua duka la Danube.
Duka hilo linalotarajiwa kuzinduliwa kesho Mlimani City litakuwa duka kubwa zaidi lililosheheni fanicha zote na zenye garama nafuu mno kwa wateja wote
mrembo huyo pia ni mzazi mwenza wa mwanamziki maarufu hapa nchini Tanzania Naseb Abdul(Diamond Plutnumz)
"Ni duka kubwa sana ambalo litakuwa na vitu mbalimbali ambalo halijawahi kupatikana kwa Afrika Mashariki na Afrika nzima, hivyo tunawakaribisha sana,"amesema.
Zari ameonyesha furahayake kwa kusema kuwa ,anafurahia sana kwa kuwa wanafunya uzinduzi wa duka hilo jipya huku ikiwa ni siku maalumu yenye kumkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere hivyo ni taswira njema zaidi ambayo italipeleka taifa katika mstari wa mbele zaidi kibiashara na uchumi.
Post a Comment