MKE WA RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA ZANZIBAR
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli kushoto akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein mara baada ya kuwasili katika nyumba ya kulelea Watoto Mazizini kwa ajili ya kusalimiana nao na kuwapa msaada wa Chakula ikiwa ni miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli akiwa amembeba Mtoto Yussuf ambae analelewa katika kituo cha Watoto Mazizini baada ya kuzaliwa na Kutelekezwa na Wazazi wake.katikati ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Maudline Cyrus Castico na wa mwisho ni Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Shadya Mohammed Suleiman.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli kushoto akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein wapili kulia na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Maudline Cyrus Castico katikati wakikabidhi msaada ya Chakula kwa ajili ya Watoto yatima wanolelewa katika Kituo hicho.Wamwisho kulia ni Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Mjini Unguja.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli akipokea Zawadi ya Mkeka kutoka kwa Mlezi wa kijiji cha kulelea Watoto SOS Mombasa Zanzibar, alipokuwa katika ziara ya kuwatembelea na kuwafariji Watoto wanaolelewa katika kijiji hicho .
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Post a Comment