WAZIRI SIMBACHAWENE KUOMBA JIJI LA DODOMA KWA RAIS JOHN MAGUFULI
Mwambawahabari
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI George Simbachawene (wa pili kushoto) akiingia katika Ofisi za
Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kukagua magari na mitambo
iliyorithiwa na Manispaa hiyo kutoka kwa iliyokuwa Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA) wakati wa ziara ya siku moja ya Waziri
huyo katika Manispaa hiyo jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
Christine Mndeme na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma
Mhandisi Lusako Kilembe.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene wakati wa ziara ya siku moja
ya Waziri huyo katika Manispaa hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma Christine Mndeme
………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Juma
Ofisi ya Mkuruygenzi wa Manispaa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI George Simbachawene ameahidi kumfikishia Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli ombi la kuitangaza Manispaa ya
Dodoma kuwa Jiji kwani inakidhi vigizo na kwamba sasa ni wakati muafaka
wa kupewa hadhi hiyo.
Alitoa ahadi hiyo jana wakati
akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Dodoma katika Ukumbi wa Shule ya
Sekondari ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika
Manispaa hiyo, iliyojumuisha pia ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo.
Aidha, amewataka watumishi wa
iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao (CDA) kumshukuru Rais kwa uamuzi
wa kuivunja Mamlaka hiyo kwa sababu hatua hiyo imeondoa mkanganyiko
uliokuwepo katika kuhudumia wananchi hususani katika sekta ya ardhi na
mipango miji ambako Manispaa ya Dodoma pia ilikuwa na jukumu hilo.
Pia aliwaeleza watumishi hao
wapatao 260 kuwa, sasa watapata fursa pana zaidi ya kuitumikia nchi yao
katika mikoa mbalimbali watakayopangiwa kuendelea kutumikia wananchi
kwani wao ni watumishi wa umma na wana haki na wajibu wa kufanya kazi
sehemu yeyote nchini.
Post a Comment