WALIMU KUENDELEA KUPATIWA MAFUNZO MAALUM YA KUFUNDISHA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU
Na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema imeandaa mtaala mpya ambao
umeandaliwa katika misingi ya elimu jumuishi ambao ulianza kutumika
kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015 ili kumudu wanafunzi wenye mahitaji
maalum.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng,Stella Manyanya wakati akijibu swali
la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Stella Ikupa Alex aliyetaka kujua Serikali
ina mpango gani wa kuhakikisha kila mwalimu anapatiwa mafunzo maalum
yatakayomwezesha kufundisha wanafunzi wenye ulemavu.
“Hadi sasa wahitimu wa ngazi ya
Stashahada ya Elimu maalum wapatao 158 wamehitimu Octoba 2016 na
wanachuo 248 wanaendelea na masomo katika chuo cha Ualimu
Patandi”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Aidha Waziri uyo amesema kuwa
kutokana na umuhimu wa walimu hawa Wizara yake katika mwaka wa fedha
2016/17 iliendesha Mafunzo kwa walimu 519 walio kazini wanaofundisha
darasa la kwanza na la pili kuhusiana na mtaala ulioboreshwa ili kumudu
ufundishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Pamoja na hayo tarehe 20 mpaka 28
Juni,2017 walimu 712 walio kazini wanaofundisha wanafunzi wenye ulemavu
wa akili na wenye usonjo walipatiwa mafunzo katika vituo vya
Mwanza,Arusha,Mbeya na Morogoro ili kuwajengea uwezo wa kumudu
ufundishaji wa wanafunzi wenye ulemavu huo.
“Walimu 600 wanaofundisha darasa
la tatu na nne watapatiwa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa kuanzia tarehe
10 hadi 30 Julai,2017 lengo ni kuwafikia wengi zaidi”Alisisitiza
Mhe.Manyanya.
Post a Comment