PICHA : DC MJEMA ASHIRIKI FUTARI KWA NIABA YA WAZIRI MKUU MAJALIWA
Na John Luhende
Mwambawahabari
Mkuuwa Wilaya ya ilala Mhe. Sophia Mjema amezitaka taasisi zote za kidini nchini kuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya kijamii na kiimani ili kuimarisha umoja na kudumisha amani na
mshikamano wa kitaifa.
Mh Mjema ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika Futari ya pamoja iliyandaliwa na Taasisi ya ya Maridhiano Tanzania amabayo illiandaliwa kwa lengo la kuwaleta pamoja madhehebu ya Dini mbalimbali kutathinini mstakabali wa amani ya nchi .
Aidha Mhe. Mjema amaesema taasisis za kidini nchini zina mchango mkubwa katika kudumisha amani ya nchi kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanawasikiliza viongozi wao wa kiro hivyo umoja wa viongozi hao utasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda amani
Kwamujibu wa waandaaji wa Futari hiyo iliyodhaminiwa na Kampuni ya Super Doll ,watu wapatao zaidi ya 400 walishisriki , ambapo wamesema utaratibu huu wa kufuturisha utakuwa endelevu na mwakani wamekusudia kufuturisha watu wapatao 1000.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema aliye upande wa kulia akiwa katika mazungumzo na moja ya wageni waalikwa katika futari iliyoandaliwa na taasisi ya Mridhiano.Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akisalimiana na baadhi ya viongozi na wageni waalikwa walio hudhuria futari katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Taasisi ya Maridhiano tanzania Osward Mlay aliyeko katikati akisalimiana na viongozi mbalimbali wa taasisis hiyo
Katibu mkuu wa Taasisi ya Maridhiano tanzania Osward Mlay aliyeko akisisistiza jambo wengine ni moja wa viongozi wa taasisis hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wageni waalikwa katika futari ya taasisi ya Maridhiano Tanzainia .
Post a Comment