Ads

NMB Bank yawezesha kufanyika kwa Kids Circus Carnival


 Mwambawahabari
 
Benki ya NMB Tanzania imeungana na Watanzania nchini kusherehekea sikuu ya Eid kwa kudhamini tamasha ambalo limehusisha watu wa aina mbalimbali kuanzia watoto n ahata watu wazima la Kids Circus Carnival.


Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa siku mbili yaani Eid Mosi (Juni, 26) na Eid Pili (Juni, 27) linafanyika katika viwanja vya Kenyatta (Kenyatta Ground) vilivyopo Osterbay, Dar es Salaam.

Katika tamasha hilo kulikuwa na huduma mbalimbali ambazo zinazotolewa na benki ya NMB ambapo watu waliohudhuria tamasha hilo walipata nafasi ya kujua huduma zinazotolewa na NMB lakini pia kupata nafasi ya kufungua akaunti.

Pamoja na hilo pia kulikuwa na michezo mbalimbali ya watoto na wanyama mbalimbali wakiwepo simba, chui, mamba, farasi, sungura na wengine mbalimbali.

No comments