MBUNGE KOKA ACHANGIA MILIONI 3 KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI YA WAISLAMU WILAYA YA KIBAHA
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini
Silvestry Koka akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu hawapo pichani
wakati wa sherehe za Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Kibaha
kwenye viwanja wa Mwendapole Wilayani Kibaha (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Naibu Sheikh wa Mkoa wa Pwani
Hamisi Mtupa akizungumza jambo wakati wa sherehe hizo za baraza kuu la
waislamu Wilaya ya Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………
VICTOR MASANGU, KIBAHA
VIJANA wa dini ya kiislmamu
hapa nchini wametakiwa kuachana na vitendo vya kushinda vijiweni na
kujiingiza katika wimbi la uhalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya
ambayo yanachgangia kwa kisi kikubwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa na
badala yake sasa wawe wazalendo kwa kuhakikisha wanazilinda kwa hali
na mali rasilimali zote pamoja na kutunza amani iliyopo
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa wakati wa sherehe za baraza kuu la
waislamu la Iddy ngazi ya Wilaya ya Kibaha ambalo limefanyika katika
viwanja vya mwendapole na kuhudhuliwa na viongozi wa ngazi mbali mbali
wa dini pamoja na serikali kutoka katika Mkoa wa Pwani.
Sheikh Mtupa mbaye pia ni Kadhi
wa Mkoa wa Pwani alibainisha kuwa kwa sasa watanzania wote wanapaswa
kubadilika na kuhakikisha kwamba wanakuwa walinzi wa rasilimali zote
zilizopo nchini kwa lengo la kuweza kuwathibiti baadhi ya watu ambao
wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe kwa maslani yao binafsi bila ya
kujali wananchi wa hali ya chini.
Hama kwa upande wake Mbunge wa
jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
sherehe hizo amewaasa wananchi wote kuunga mkono juhudi zinazofanywa
na Rais Dk John Magufuli pamoja na kuchapa kazi kwa bidii ili kuweza
kupambana na janga la umasikini na kuachana na kuwa tegemezi ambapo pia
amechangia kiais cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
ya waislmau ya Wilaya.
Koka alisesema kwamba nia yake
kubwa ni kushirikiana na wananchi wa jimbo lake katika kuleta maendeleo
hivyo amewaomba waislamu waendelee kujenga upendo na ushirikiano wa hali
na mali katika kuakikisha kwamba ujenzi wa ofisi hiyo ya wilaya
inakamilika ili iweze kuanza kufanya kazi kwa jili ya kutoa huduma.
“Mimi kama mbunge wenu katika
hili kwa kuanzia nitachangia kiais cha shilingi milioni tatu lakini sio
kwamba ndio nitaishia hapo hapana nataka kuona na nyinyi wenzangu
tunashirikiana kwa pamoja ili kuweza kukamilisha ujenzi wa ofisi ya
Wilaya na nikiona kwamba tupo pamoja na mimi tena nitaongezea kiasi cha
shilingi milioni mbili lengo ikiwa ni kuona tunakuwa na sehemu sahihi ya
kuweza kukutana na kufanya shughuli zenu,”alisema Koka.
Awali akisoma risala katika
sherehe hizo Katibu wa kamati ya maandalizi ya Baraza la Iddi Wilaya ya
Kibaha Hoseni Ibrahimu ameiomba serikali ya awamu ya tano kuongeza
vipindi vya dini mashuleni kwa lengo la kuweza kutoa huduma za kiroho
kwa wanafunzi wa kiislamu
“sisi kama baraza kuu la
waislmamu Bakwata Wilaya ya Kibaha kikubwa tunachoiomba serikali ni
kuongeza vipindi vingi vya dini katika mashule ili wanafunzi waweze
kupata fursa ya kujifunza zaidi mafundisho ya kiroho na tuna imani
itaweza kusaidia kuwaongezea uwezo mkubwa katika kujifunza mambo mbali
mbali yanayohusina na dini ya kiislamu,”alisema Ibrahimu.
BARAZA kuu la waislamu (BAKWATA)
Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa licha ya kukabiliwa na
changamoto mbali mbali linahitaji kiasi cha shilingi milioni 15 kwa
ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa ofisi ya wilaya.
Post a Comment