Ads

UTOAJI MIMBA USIOSALAMA WACHANGIA 15 YA VIFO VYA WANAWAKE NCHINI


Image result for NEMBO YA TAWLA


UTOAJI wa  mimba usio salama  inachangia asilimia 13 hadi 15 ya vifo vingi vya
uzazi kwa wanawake ambayo ikishughulikiwa itasaidia kupunguza vifo vya kina
mama vinavyotokana na uzazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwandisi Mwandamizi
wa Afya ya jamii katika chuo cha Kairuki Pasiens Mapunda wakati wamkutano
ulioandaliwa na chama cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) alisema
kuna vifo vingi vya uzazi hapa nchini.

" Utoaji wa mimba unaoendelea unatolewa kwa kificho na wanatolewa na watu
wasio na ujuzi wa kutoa hali hiyo inasababisha madhala mengi sana ambayo
baadaye yanasababisha vifo vya uzazi na inabidi kupambana ili kuweza
kuondokana na tatizo hilo" alisema Mapunda.

Alisema sehemu ambazo matumizi ya uzazi wa mpango ni mdogo sehenu hizo
zinaongoza kwa mimba zisizotarajiwa ambayo na kuchangia ongezeko  kubwa la
utoaji mimba kwa  wanawake ambapo imeonekana wanawake kuanzia miaka 15
hadi 49 ndio wanaotoa mimba.


Alisema kwasababu ya uoga wa dini na sheria za nchi ni vizuri kukawa na
mazungumzo ua kuzuia utoaji wa mimba na kuangalia namna ya kuwasaidia
wanawake wanaobakwa na wale wanaoingiliwa na wazazi wao bila makubaliano.

"Utoaji mimba una madhara makubwa kwa uzazi wa mwanamke inatakiwa
kutafuta njia ili kuweza kudhibiti mambo haya yasitokee ndomana
tumechanganyika katika mkutano huu na wanasheria na wadau mbalimbali ili
kupiga vita matatizo haya ili kupunguza vifo vya uzazi vya kina mama" alisema
Mapunda.

Alisema zile mimba zinazopatikana kwa udhalilishaji kama kubakwa, na
kuingiliwa na mzazi ziruhusiwe kutolewa kisheria na bunge letu na lipo kwenye
mazunumzo.

Alisema jinsi ya kupinguzani kuhakikisha kuwa  mimba azitarajiwi lazima kuwepo
na njia ya kuzuia mimba hizo kama kutumia njia za uzazi  wa mpango na kupewa
ushauri ya namna ya kupanga uzazi salama ili kuepuka mimba zisizotarajiwa.
Alisema Tanzania hakuna sheria inayoruhusu mimba kutolewa ila inaruhusiwa
pale inapohitajika kwaajiri ya kuokoa maisha ya mama endapo daktari ataona
kuna tatizo kwa mama mjamzito.

Alisema yapo madhara makubwa ambayo anayapata mwanamke pale anapotoa
mimbaikiwa ni kutoka damu nyingi, kutoboa kizazi au matokeo ya kuziba kwa
kizazi ambapo mwanamke anaweza kukosa mtoto pale atakapokuwa anahitaji
kuzaa.
Alisema wanaohusika kwa kitendo cha utoaji mimba ikiwemo mama mjamzito,
daktari atayehusika kutoa pamoja na mpeleka vifaa adhabu yao ni kubwa ikiwa
ni kifingo cha miaka 14 kwa mtoaji.

No comments