NHC YATEKELEZA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA 30,000
Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC ),Erasto Chilambo (kushoto) akijibu maswali kwa waandishi wa habari (kulia) Meneja wa Mawasiliano wa Shirika hilo, Yahaya Charahani.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON
Na. Jesca
mathew
mwambawahabari
Tatizo la
upatikanaji wa ardhi nchini limekuwa ni tatizo kubwa kwa taifa jambo
linalosababisha wananchi wa kipato cha chini kushindwa kumudu gharama za umiliki
wa nyumba.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini dar es salaam meneja masoko wa shirika la nyumba
la taifa NHC Erasto Chilambo amesema changamoto hiyo inazidi kuongezeka kwa
kuwa gharama za maisha zinazidi kupanada na kufanya gharama za ujenzi
kuongezeka.
'' lengo la
shirika la nyumba ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kumiliki
nyumba hivyo upatikanaji wa ardhi ungekuwa wa bure ingerahisisha gharama za
ujenzi kupungua na kufanya kila mtanzania mwenye kipato cha chini kumiliki
nyumba .''alisema chilambo.
Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC ),Erasto Chilambo (katikati) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo akielezea utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba ya Shirika hilo ( kushoto), Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) Bi Edith Nguruwe, Meneja wa Mawasiliano wa Shirika hilo, Yahaya Charahani.
Meneja huyo
akaongeza kuwa shirika la nyumba limeandaa mkakati wa kujenga nyumba elfu
thelathini za kuuza na kupangisha ifikapo mwaka 2025 ikiwa ni mkakati wa miaka 10 ulionza mwaka 2015.
''tumekusudia
kujenga nyumba elfu 12 kwa ajili ya watu wa kipato cha chini,13,500 elfu za
watu wa kipato cha kati na nyumba elfu 2,700 kwa ajili watu wenye kipato cha
juu.''aliongeza chilambo.
Post a Comment