Ads

TUCHANGAMKIENI FURSA DUNIANI KOTE: RAIS MAGUFULI


Displaying 14.jpg

Na. Immaculate Makilika 
mwambawahabari
Watanzania wametakiwa kujishughulisha  katika  shughuli  za kujiletea  maendeleo kwa kutumi fursa zinazopatikana katika  maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo, Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alisema kuwa watanzania wanakila sababu ya kujipatia maendeleo kwa vile wamezungukwa na fursa mbalimbali ikiwemo kuwa mwananchama wa  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) ambapo wanaweza  kutumia fursa hiyo ili kujiletea maendeleo.


“Wito wangu kwa watanzania ni huu tuchangamkieni fursa duniani kote, kwa vile watanzania tuna uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha, tumesoma vizuri na tunaweza kufanya ujasiriamali, hivyo tunaweza kutumia fursa zilizopo katika soko la jumuiya ya SADC yenye nchi 15 na nchi 6 za jumuiya ya EAC” alisema Rais Magufuli
Mbali na hayo, Rais Magufuli amezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo fursa za uwekezaji kwa   watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora) ambapo amewataka  kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza kwa vile serikali imejiandaa kuhakikisha kunakuwepo na mazingira yanayovutia  wawekezaji nchini.

“Tunawakaribisha wageni kutoka nchi mbalimbali duniani kuja kuwekeza, kwa hiyo  hata  watanzania wanaoishi nje ya nchi tunawakaribisha  kuja  kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji” alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amewataka wahariri pamoja na waandishi wa habari kutumia taaluma yao katika kuleta chachu ya maendeleo kwa kuandika na kutangaza habari zenye kumjenga mtanzania na kusisitiza kuwa wazalendo pamoja na kuweka mbele maslahi ya Taifa kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae.

No comments