WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA TOTO ATOA UFAFANUZI KUHUSU UPUNGU WA DAWA NCHINI
Mwambawahabari
Na Maria Kaira Dar
Vituo vya kutolea huduma za Afya nchini vimehimizwa kupeleka mahitaji na maoteo yao muhimu ya dawa katika bohari kuu ya dawa (MSD) ili kuondokana na adha ya ukosefu wa dawa kwenye vituo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati Wa ufafanuzi wa upatikanaji dawa nchini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema vituo vya afya wanatakiwa kutoa taarifa mapema sio hadi wasubiri dawa ziishe ndio watoe taarifa sehemu husika.
Ummy amesema wizara ya afya inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa itasimamia ipasavyo utapatinaji wa dawa na vifaa tiba nchini kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kuwa Sera ya afya inawataka wananchi kuchangia huduma.
Aidha amesema ili kuondokana na vikwazo kwa wananchi kupata dawa na huduma za afya kwa ujumla, wananchi wanahimizwa kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya ili iweze kuwasaidia wakati wanapokuwa hawana akiba ya fedha, ila ukiwa na bima wakati wowote unapata matibabu.
"Hivyi karibuni kumekuwepo na taarifa zilizodai kwamba katika kipindi hiki kuna upungufu mkubwa wa dawa katika bohari kuu ya dawa , Hivyo, kusababisha kukosekana kwa dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya taarifa hizo sio sahii na zinalenga kupotosha umma na kuwatia wananchi wasiwasi" amesema
Waziri Ummy amesema upatikanaji wa dawa kwa sasa uko vizuri na dawa muhimu zinazohitajika sana nchini zinapatikana kwenye maghala ya Bohari ya Dawa (MSD).
"Mfano kwa upande wa dawa za antibiotics tuna Amoxycillin, Ciprofloxacin, Cotrimoxazole na Doxycycline. Kwa upande wa dawa za maumivu – tunazo za kutosha kama vile paracetamol, asprin na diclofenac. Pia tuna dawa za kutosha za malaria, Kifua Kikuu, ukoma na dawa za kufubaza makali ya UKIMWI (ARVs)" amesema
"Kwa upande wa chanjo za watoto na wajawazito, ni kweli kulikuwa na uhaba nchini kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita hata hivyo, wiki iliyopita Serikali imenunua na kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya Kifua Kikuu (BCG), dozi milioni 1.2 za Polio na dozi milioni za Polio" amesema
Hata hivyo dawa nyingine zitaendelea kupatikana katika Bohari kuu ya Dawa kwa kuwa tumeagiza dawa za kutosha kutoka kwa wazalishaji wa ndani na nje ya nchi.
Post a Comment