Ads

WATANZANIA MILIONI 47 HATARINI KUUGUA MAGANJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE.



Na Maria Kaira 
Mwambawahabari
Ofisa mipango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Oscar Kaitaba kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amesema watu milioni 47 nchini wapo hatarini kupata magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na kusababisha nguvu kazikupotea.

Magonjwa hayo ni pamoja na Matende  Kichochona Minyooo, pia watu milioni 200 wanakabiriwa na kichocho huku watu elfu 20 kwa mwaka dunianihufariki dunia kwa ugonjwa wa kichocho, huku watu milioni 4 wapo hatarini kupata ugonjwa wa Usubi.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Ofisa huyo wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele amesema matarajio yao ya mpango huo ni kuhakikisha wanakabiliana na magonjwa hayo nchini na kuwapa elimu wananchi kuhusu magonjwa hayo faida na hasara sake.


Aidha kaitaba amesema  watu milioni 47 wapo hatarini kupata ugonjwa wa minyoo kutokana na kula vyakula visivyokuwa visafi, pia akatoa ushauri kwa jamii kuwa wasafi kwa vyakula wanavyovitumia.

Ameongeza kuwa katika mpango wa kudhibiti magonjwa hayo, Oktoba 25 hadi 30 mwaka huu katika mkoa wa Dar es Salaam kutakuwa na ugawaji wa dawa za kingatiba za Minyoo ya tumbo ,matende na mabusha ambazo zitatolewa katika vituo maalum vilivyoteuliwa.

“Kingatiba hizo zitatolewa bure kwa jamii na hazina madhara yoyote mwananchi asiogope kuzitumia mana zimedhibitishwa na mamlaka ya dawa na chakula ,pia ukienda katika vituo vyetutulivyoviweka ni pamoja na Stendi za mabasi , masoko, hospitali, ofisi za serikali za mitaa, ofisi za Wizara, taasisi lazima utapata kinga"alisema Kaitaba.

Hata hivyo alizitaja aina za dawa za kingatiba hizo ambazo zitatolewa kwa jamii ni pamoja na Albendazole na Ivermectim,walengwa ni wananchi wote kuanzia miaka mitano na kuendelea isipokuwa wajawazito na watu ambao ni wagonjwa mahututi.

"Tutafanya upasuaji kwa watu 400 wenye mabusha katika manispaa ya Ilala ambao utafanyika katika Hospitali ya Pugu Kajiungeni hivi karibuni tunaomba wananchi kujitokeza kwa wingi na kuachana na mila potofu mabusha tunayafanyia oparesheni na unakuwa safi" amesema

" lengo letu ni kutokomeza haya magonjwa na hasa ni kuwataka wananchi kuelewa mapema matatizo yanayotokana na magonjwa hayo napenda kuwatoa hofu wananchi kujitoa kwa wingi Siku hiyo" amesema

No comments